Tume ya uchaguzi nchini venezuela imetangaza
kiongozi wa kisoshalisti Nicolas Maduro kama mshindi wa uchaguzi wa urais kwa
asilimia 51 tu ya kura.
Hata hivyo ushindi huo dhidi ya mpinzani wake mkuu
Henrique Capriles ulikuwa ni wa chini ya asilimia mbili, ikiwa ni chini ya robo
ya kura zipatazo milioni 15 ya zile zilizopigwa .
Ni ushindi mdogo zaidi ikilinganishwa na ule
alioupata kiongozi wa chama chake hayati rais Hugo Chavez,mwaka jana, muda
mfupi kabla ya kifo chake.
Kufuatia tangazo la ushindi huo Bwana Maduro
alivaa mavazi yenye rangi za bendera ya Venezuela akidai uchaguzi wake ni wa
haki na wa kisheria na akawataka raia wawe watulivu. Aliahidi kuendeleza sera
za Bwana Chavez.
Pindi habari zilipojitokeza kuwa Maduiro alikuwa
mshindi, wafuasi wake walianza kusherehekea mjini Caracas, huku wafuasi wa
upinzani nao wakianza kupiga sufuria kuonyesha ghadhabu zao.
Katika hotuba yake ya ushindi akiwa nje ya ikulu
ya rais, bwana Maduro, aliambia wafuasi wake kuwa ushindi wake ni halali na
umeambatana na sheria. Aliongeza kuwa kuchaguliwa kwake kunaonyesha kuwa
marehemu Hugo Chavez anaendelea kushinda vita vikuu.
Aliwataka wale waliompigia kura na wapinzani wake
kushirikiana kwa niaba ya ya nchi nzima.
Source bbc swahili



Post a Comment