TUNAOMBA RADHI
KWA KUWALETEA TAARIFA NDEFU KIASI HIKI KWANI MNATAMBUA KUWA SERA ZETU NI KUTOA
TAARIFA KWA UFUPI TU, LAKINI KUTOKANA NA UNYAMA, UKATAILI ALIOFANYIKA MTOTO
HUYU,HABARIMPYA.COM IMEAMUA KUWALETEA TAARIFA HII KWA UNDANI ZAIDI HIVYO
TUNAOMBA UISOME KWA UMAKINI MKUBWA MWANZO HADI MWISHO.
UKICHOKA PUMZIKA NA URUDI BAADAYE KWANI ITAENDELEA KUWA HAPA KWA ZAIDI YA WIKI NZIMA BILA KUPOTEA.HABARIMPYA.COM PIA INALAANI TUKIO HILI KWA NGUVU ZOTE, TUNAOMBA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE ILI IWE FUNDISHO KWA WATU WENYE TABIA ZA AINA HII, MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN.
Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai wake
Riziki Mwangoka kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai
Hapa maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya nyumba ya baba yake mzazi
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI TUNAZOZIONYESHA
Mwili wa marehemu Debora ukionyeshwa kwa mzazi na kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia
Mwili wa mtoto Debora ukiandaliwa kwa kuzikwa kwa heshima zote
Mwili wa Debora tayari kwa kuzikwa
Hatimae sasa Debora anazikwa
Mara tu baada ya mazishi baba mzazi wa Debora anapelewa kituo cha polisi Tukuyu
Mama mzazi wa marehemu Debora asimulia kisa chote
Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili
Bibi wa marehemu Debora
Tukiwa na baadhi ya waandishi wenzangu tukiendelea kupata historia fupi ya marehemu Debora toka kwa mama yake mzazi
Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
Dada wa
marehemu Debora, Neema Stevini(5) kulia ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi
wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbuka
mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.
“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia
nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia
sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema.
MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai
kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa
marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .
Akizungumza kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu
na Mbeya yetu kijijini kwake Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe,
Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea
kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili.
Alisema tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto na
kwenda kumfanyia ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali
kumuiba akiwa na miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya
serikali ya kijiji.
Alisema katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo
kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za
kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola,
kijiji cha Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.
Alitaja sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana
na yeye kuhoji sababu za kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na
wao kwa pamoja kufanya kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada
ya malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha
sh.80,000.
Alisema ugomvi huo ndio ulisababisha yeye arudishwe
kwa wazazi wake, lakini baada ya muda mfupi mwanaume huyo alimfuata na
kumbembeleza ili warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto
.
“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi
kuondoka nyumbani kwake na kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa
shambani huyo bwana alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema
Steven ) niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja.
Alisema baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili
asubuhi alitumia ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye
kijijini kwao Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi
Kiwira.
“Unajua kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi
walitusaidia kufika kijijini kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue
mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa
chini ya miaka saba”.
Aliongeza kuwa Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya
kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo
wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku
ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha
miaka saba.
Tukio la pili la kuiba mtoto.
Alisema tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana
2012, ambapo alifika nyumbani kwao majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa
marehemu kumchukua mtoto akimdanga kuwa anaenda kusenya kuni eneo la
jirani.
Aliongeza kuwa baada ya kuona dada wa marehemu
anang’ang’ania kwenda wote alimuamuru arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa
kulikuwa kumeinjikwa mboga na kukubali kurudi.
“kwa mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza
alisema baada kurudi toka ndani, alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na
tuliporudi na kupokea taarifa hizo tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo”
alisema mama wa marehemu.
Mwambenja alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili
asubuhi yake walienda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kiwira ili waweze
kupata msaada wa kumtafuta, huku wakionesha barua ya makubaliano ya awali ya
yeye kuwa na haki ya kisheria ya kusimamia malezi ya mwanao hadi afikishe miaka
saba.
Alisema baada ya kutoa taarifa hizo kituoni hapo,
askari aliyekuwa zamu siku hiyo alimtaka kutoa kiasi cha shilingi 50,000 ili
fedha hizo wapewe askari mgambo wa kwenda kijijini kwa mzazi mwenzake huyo,
kwani tayari walikuwa na taarifa kuwa alikuwa amekimbilia
huko.
“Kutokana na hali ngumu ya maisha tulikosa kiasi
hicho cha fedha hivyo suala hilo kubaki bila msaada wa polisi na pia
hatukuweza kwenda kwa kijijini kwao”.
Aliongeza “sababu ya mimi kuwa mzito kuendelea
kumfuatilia kijijini kwao kwa mara ya pili ili kujua kama yupo huko na mtoto
ilitokana na hofu niliyoijenga, kwani awali tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno
ya vitisho kuwa endapo nitaendelea kung’ang’ania kumchukua mtoto pale
anapomchukua atakuja kumuua ili tukose wote”.
Hata hivyo mama huyo mzazi wa Debora, alisema kuwa
baada ya kuona hali hiyo, aliendelea kuwasiliana na wifi yake , Bupe
Mwangoka,ambaye ni dada mkubwa wa mume wake anayeishi eneo la Isanga Jijini
mbeya, ambaye ndiye alisaidia kwa kiasi kikubwa kubainika kwa unyama
aliofanya.
Maisha
kabla ya tukio.
Akielezea maisha yao kabla ya kutengana na baadae
kuamua kufanya ukatili huo, alisema aliwahi kumtamkia maneno makali wakati akiwa
na ujauzito wa miezi nane .
Alisema baada ya kuibuka ugomvi katika kipindi hicho,
mwanaume huyo alimtaka kwenda kuiuza mimba ile kwa mwanaume mwingine yeyote
atakayempenda ili asije akazaa mtoto ambaye atachanganya damu ya koo hizo
mbili.
“Maneno yale katika kipindi hicho sikuyatilia maanani
kwani nilifikiri zilikuwa ni hasira, lakini leo hii ndio najua maana ya ile
kauli ” alisisitiza Mwambenja.
Hata hivyo alisema inashangaza kwani kuna wakati
tukiwa katika maisha ya kawaida kabla ya yeye kufanya tukio hilo, mara kadhaa
alijutia na kuonya juu ya matukio machafu yaliyojitokeza na kusikika ya watu
kuuawa au kuondolewa baadhi ya viungo vya miili yao.
Aidha, alieleza mkasa mwingine wa mume wake huyo ni
ule wa wao kufukuzwa katika mji wa Kiwira walikokuwa wakiishi awali kwa kufanya
shughuli za umachinga.
Alisema walitimuliwa na serikali ya mtaa katika mji
huo kutokana na mumewe huyo kutuhumiwa kuiba simu ya mkononi ambapo alipokea
kipigo kikali na baadae kufukuzwa.
Kutokana na hali hiyo, mama wa marehemu Debora
alisema yote yaliyotokea amemwachia mungu na kwamba kama ingekuwa uwezo wake
angeamuru naye anyongwe, hivyo mamlaka husika zitajua cha
kufanya.
Kwa upande wake dada wa marehemu Debora, Neema
Stevini(5) ambaye ni mtoto wa kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia
jinsi mdogo wake alivyoibwa , alisema kuwa anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa
jioni majira ya saa 12 jioni.
“Nilitaka kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia
nirudi kuchochea moto ndani na niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia
sana siku waona” alisema kwa masikitiko Neema.
Hata hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa
marehemu Debora alifariki dunia siku hiyo ya Novemba 29 mwaka jana, majira ya
saa nne usiku baada ya baba yake kufanikiwa kumuiba kutoka nyumbani kwa mama
yake.
Inadaiwa kuwa baada ya kufanikiwa kumtorosha baba
huyo wa marehemu alitembea kwa mguu umbali wa kilomita 50 kutoka kijiji cha
Ibula alikomuiba hadi nyumbani kwake kijiji cha Isange katika kata ya
Isange.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, baba
huyo mzazi wa marehemu alichimba shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto
wake huyo akiwa usingizini na kisha kumfukia akiwa hai.
Mwanaume Yule alikuwa katili sana, kwani baada ya
kumfukia alichukua meza ya chakula na kuiweka juu yake huku akiipamba kwa
magazeti jambo ambalo lilifanya ndugu zake wasigundue kirahisi” alisema mpasha
habari.
Chanzo hicho kilisema baada ya kufanya hivyo aliishi
kwa wiki moja na baadae kukimbilia Jijini Mbeya ili watu wasibaini juu kitendo
alichofanya na kwamba kila alipohojiwa na ndugu zake alisema mwanae huyo
alimuweka kwa rafiki yake Jijini Mbeya.
Hata hivyo baada ya danadana za muda mrefu ndipo dada
wa mtuhumiwa huyo aliamua kutoa taarifa jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata
akiwa katika harakati za kutorokea wilayani Chunya na alipobanwa alifichua siri
ya alipo mwanae kwa kueleza kuwa alimuua na kumfukia ndani
kwake.
chanzo habari mpasuko
Post a Comment