Majid Mjengwa.
***********
MWANDISHI
wa safu katika magazeti mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na polisi
kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Habari zilizoufikia mtandao huu jana mchana na baadaye
kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba
alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la
kuteswa kwa Kibanda.
Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso alisema
kwamba:
“Ni kweli kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji,
tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo
lolote tutawajulisha.”
Hata hivyo,
Senso hakuwa tayari kueleza kwa undani muda aliokamatwa Mjengwa wala sababu za
kukamatwa na kuhojiwa kwake, lakini chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi
kilithibitisha kwamba pamoja na mambo mengine kuhojiwa kwake kulihusu uteswaji
wa Kibanda.
Jumatatu wiki hii, Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
Nchini, Issaya Mngulu alisikika akizungumza na Kituo cha Radio One cha Dar es
Salaam kwamba kesho Jumatatu (April 15, 2013) polisi watatoa taarifa rasmi ya
hatua waliofikia katika upepelezi wa kesi ya Kibanda.
Kwa upande wake Mia Mjengwa ambaye ni mke wa Mjengwa,
alisema mumewe alipata wito kutoka polisi makao makuu Alhamisi na kwamba juzi
Ijumaa alisafiri kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam kuitikia wito
huo.
“Ninachojua ni kwamba aliitwa kwenda polisi na leo
(jana) alinipigia simu kama saa 7:00 mchana na aliniarifu kwamba yupo polisi,
sasa tangu wakati huo sijaongea naye tena na wala simu zake hazipatikani,”
alisema Mia na kuongeza: “Kwa hiyo mimi kwa kweli sifahamu kwamba anahojiwa kwa
sababu gani.”
Taarifa za kukamatwa kisha kuhojiwa kwa Mjengwa ambaye
pia ni mmiliki wa Mjengwa Blog, zimekuja siku chache tangu msaidizi wake katika
Blog hiyo, Joseph Ludovick akamatwe, kuhojiwa kisha kufikishwa mahakamani kwa
tuhuma za ugaidi.
Ludovick alifikishwa mahakamani pamoja na Mkurugenzi wa
Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willifred Lwakatare
wakikabiliwa na tuhuma za ugaidi na kupanga kumteka Mhariri Mtendaji wa
Mwananchi, Dennis Msacky.
Kuteswa Kibanda.
Machi 5, mwaka huu saa 5.30 usiku, Kibanda ambaye pia
ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alinusurika
kifo baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake kisha kupigwa na
kujeruhiwa vibaya.
mwananchi
mwananchi
Post a Comment