Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwekezaji wa China kujenga lodge Serengeti


chinese b4bbc
Balozi wa Tanzania nchini China Philip Marmo akiongea na mwekezaji Zhou Yi (wa pili kushoto) ofisini kwake jijini Beijing China. Wengine katika picha ni Pan Lei, Mkurugenzi wa Kampuni ya kichina ya Fashion Tourism yenye ofisi yake nchini pamoja na Allen Lee kutoka Chama cha Mawakala wa Utalii Beijing, China.
MILIONEA wa Jamhuri ya Watu wa China, Zhou Yi anatarajia kujenga loji kubwa ya kisasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Zhou alisema hayo jana jijini Beijing nchini china alipokutana na ujumbe wa serikali ya Tanzania unaotembelea China kwa lengo la kutangaza utalii na kutafuta wawekezaji katika sekta ya utalii nchini.
Zhou anamiliki mtandao wa makampuni tanzu yanayofahamika kama Hengxu Group of Companies yenye makao makuu yake katika mji wa viwanda wa Sichuan na ameajiri watu zaidi ya 7,000 na ana mtaji wa zaidi ya dola za kimarekani milioni mia saba alisema kuwa alitembelea hifadhi ya Serengeti mwezi Machi mwaka huu na kuvutiwa sana na uzuri wa uasili uliopo Serengeti.


Alisema kuwa hivi sasa yuko katika hatua za awali ya kuomba kupatiwa eneo la kuwekeza ambapo ujumbe wa serikali unaoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao ulimuhakikishia upatikanaji wa eneo hilo ili kupunguza tatizo la uhaba wa vitanda kwa wageni nchini.
Ujumbe wa Tanzania uko nchini China kuhudhuria maonyesho maarufu ya utalii ya COTMM katika jiji la Beijing pamoja na kuandaa semina kwa wawekezaji wa China na Wamiliki wa kampuni za Utalii kuhusu vivutio vya utalii nchini pamoja na kuainisha fursa zilizopo za uwekezaji katika sekta ya utalii nchini. Semina hizi zinazofanyika katika miji ya Shanghai, Beijing na Guangzhou zinalenga kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji kutoka China nchini.
Mapema Balozi wa Tanzania nchini China na Bi. Millao waliwahakikishia washiriki kuwa Tanzania ni eneo zuri kuwekeza kwa sasa hasa kwa kuwa na vivutio vingi ikiwa ni nchi ya pili duniani baada ya Brazil. Aidha, wawekezaji hao walihamasishwa kuchangamkia fursa zilizopo hasa kutokana na utulivu wa amani uliopo nchini. Chanzo: Pascal Shelutete
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top