Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika
makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye
mazungumzo rasmi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans
akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu
wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha mbegu bora za
mazao ya mboga ya Rijk Zwaan Bwana Kees Reinink akimuonesha Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete baadhi ya miche inayotokana na mbegu bora wakati Rais
alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo katika kitongoji cha De Lier nje
kidogo ya jiji la The Hague,nchini Uholanzi jana. Wapili kushoto ni Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Bwana Geoffrey
Kirenga.Kampuni ya RIJK ZWAAN tayari imewekeza nchini Tanzania huko Arusha
ambapo inazalisha mbegu bora za mazo ya mbogamboga zilizofanyiwa utafiti
kudhibiti magonjwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa
Kampuni ya Utafiti na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana
katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague.
Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Malkia Beatrix wa
Uholanzi wakati walipomtembelea Malkia huyo katika makazi yake Rasmi jijini The
Hague jana.Rais Kikwete yupo nchi Uholanzi kwa Ziara
rasmi.Picha na Freddy Maro


Post a Comment