Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya
klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Ridhiwani alisema katika uteuzi
wa Kamati hiyo, amezingatia utaalamu, uzoefu na mahusiano mazuri.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Issa Hajji Ussi ambaye ni Makamu
wake na wajumbe ni Isaac Chanji, Mbaraka Igangula, Jaji John Mkwawa, ambaye
anafanya kazi Beki ya Uwekezaji Tanzania (T.I.B.), Alan Magoma, ambaye ni
Mwanasheria mkongwe, Mavale Msemo na Charles Palapala.
“Utaona kuna watu wengi wa taasisi za fedha ni kwa sababu
zoezi hili linahitaji fedha hivyo tutaangalia kama tutaingia ubia na mtu, au
sisi klabu tukawekeza kwenye mradi huo moja kwa moja,”alisema.
Kwa upande wa watendaji, Ridhiwan alisema kwamba Kamati yao
itaongozwa na Katibu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako, Beda Tindwa na Mahmoud
Milandu.
“Kamati yetu sisi itakuwa ya kukaa na kutengeneza mipango
na baadaye kama kutakuwa na barua ya kupeleka wapi, au mtu wa kufuatwa, basi ile
kamati nyingine ndogo, itafanya kazi hiyo,”alisema
HABARI LEO


Post a Comment