Taarifa
kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo
kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya
kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam .
Mwandishi wetu
kutoka Tunduma mkoani Mbeya anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya
saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu
uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa
wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa
pasaka.
Hata hivyo
inaelezwa kuwa vurugu hizo za leo zina mikanganyiko mingi kwani
wanaoshiriki katika vurugu hizo ni vijana wapiga debe
.....
Vurugu za
uchinjaji zilifanyika siku ya Pasaka na hazikuwa na mvutano kwa sababu
wakristo walichinja katika bucha zao na waislamu nao walichinja katika
mabucha yao ....
Cha kushangaza leo
ni baada ya kuibuka kundi la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe
mbali mbali ambao ndio walioanzisha vurugu kiasi cha polisi kuingilia kati
kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika
maeneo mbali mbali .
Kutokana na vurugu
hizo mpaka wa Tunduma ambao unaingia nchi za kusini mwa Tanzania ulifungwa
pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka Sumbawanga pia yalizuiwa kuendelea na
safari hadi hali hiyo ilipotulia mida ya saa 8 mchana baada ya kamanda wa
polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kufika eneo
hilo
Post a Comment