Mji wa
Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina yake, pale mwanamke
ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano iliyopita alipoonekana akiwa hai
katika eneo la Kasamwa.
Inadaiwa
kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya
ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi
alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James,
anayeishi Kasamwa.
Aliyekuwa wa
kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya kuamka
saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi
nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada
yake.
“Baada ya
kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada (Monica)
ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba nimeamka na kumkuta
mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia anafanana na marehemu dada
yetu,”alisema Jubili na kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka
nje.
Alisema mtoto
wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba
walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali
ya Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa
ini.
Rebeka ambaye
ni mtoto wa nne wa Flora alisema: “Mama mdogo alituita sisi tulikuwa tumelala
akasema kwamba nje kuna mwanamke ambaye anafanana na marehemu mama yetu, ndipo
na sisi tukatoka na kweli kumwangalia alikuwa ni yeye kabisa.”Alisema walipomuhoji mama yake huyo kwamba ametokea
wapi, aliwaeleza kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga na aliletwa na watu
ambao hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya gari na watu hao walimshusha
kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni jirani na dada zake
hao.
Kauli ya
Flora
Akizungumza na waandishi wa habari, Flora alisema
yeye ni mkazi wa Katoro na kwamba alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi
ambaye hata hivyo hakumtaja kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini)
wamemkataza.“Nilikuwa naishi kwa mganga
wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati nikiwa pale akaninywesha dawa kisha
tukapakizwa kwenye gari na watu wawili ambao sikuwatambua, mmoja mwanamke na
mwingine mwanaume mpaka hapa Kasamwa tukashushwa saa 1:00 jioni,”alisema
Flora.
Alisema
alipofika Kasamwa alikwenda kunywa uji kwa mama mmoja ambaye pia hakumtaja na
kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine saa nne usiku, lakini watu
wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia: “Hapa si kwako twende tukupeleke kwa
ndugu yako” na ndipo wakampeleka kwa dada yake ambako aliketi nje hadi
alfajiri.
Flora alisema
kabla ya kuishi kwa mganga alikuwa akiishi porini ambako alitupwa na watu
asiowafahamu na baadaye aliokotwa na wasamaria wema ambao ndiyo walimpeleka kwa
mganga ambako alikuwa akiishi muda wote
Post a Comment