Mkazi wa kijiji cha Kibwaya tarafa ya Mkuyuni wilaya ya
Morogoro Vijijini, Agness Aidani akiwa amepakata kichanga chake mara baada ya
kujifunguaa katika mkesha wa pasaka katika wodi ya wazazi hospitali ya mkoa wa
Morogoro ambapo jumla ya watoto 15 wamezaliwa katika mkesha huo katika Manispaa
ya Morogoro.
Mhashamu askofu wa jimbo kuu la Morogoro Telesphol Mkude
akitoa baraka wakati wa ibada ya pasaka katika kanisa kuu la St Patrick mkoani
Morogoro.
Mchungaji wa kanisa kuu la KKKT usharika wa Bungo mkoa wa
Morogoro, George Pindua akimbatiza mtoto wakati wa iabada ya ubatizo
iliyofanyika katika kanisa hilo mkoani Morogoro.
Kichanga kikiwa
kimelala katika wodi ya wazazi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro mara baada
ya mama yake kujfungua katika mkesha wa Pasaka.
Mkazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro Rehema Hassani akiwa
amelala na kichanga chake mara baada ya kujifungua kwa njia ya operesheni katika
mkesha wa pasaka katika wodi ya wazazi hospitali ya mkoa wa Morogoro ambapo
jumla ya watoto 15 wamezaliwa katika mkesha huo katika Manispaa ya
Morogoro.
Mfanyabiashara akuza mbuzi katika mitaa ya Manispaa ya Morogoro.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMLA ya watoto 22 wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Pasaka katika kituo cha Afya Mafiga na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili Muuguzi Kiongozi wa zamu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Yohana Sohaba alisema kuwa katika hospitali hiyo jumla ya watoto 15 wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Pasaka ambapo kati ya watoto hao 11 wamezaliwa kwa njia na wanne wamezaliwa kwa njia ya operesheni.
Sohaba alitaja jinsia ya vichanga hivyo kuwa ni wa kiume ni sita na wakike ni vichanga tisa na kati ya wazazi hao 11 walijifungua kwa njia ya kawaida na wanne walijifungua kwa njia ya operesheni baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
“Katika mkesha wa mwaka huu jumla ya watoto 15 wamezaliwa na kati ya hao wakiume sita na kike tisa na kati ya wazazi 15, 11 wamejifungua kwa njia ya kawaida wakati wanne wenyewe walijifungua kwa njia ya operesheni baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na afya zao wote wanaendelea vizuri na baadhi yao tayari wameruhusiwa kasoro hawa waliojifungua kwa operesheni.” Alisema Sohaba.
Katika kituo cha afya cha Mafiga jumla ya watoto saba wamezaliwa katika mkesha huo huku wakiume wakiwa tano na kike wawili ambapo wote wamejifungua kwa njia ya kawaida.
Credits: Juma Mtanda Blog
Post a Comment