ROBO FAINALI – EP1 winners & hype EP 2
*Washiriki bora kutoka Afrika wataingia katika robo fainali ya pili kuwania kufuzu nafasi ya nusu fainali*
Aprili 25, 2013, Dar es Salaam; Robo fainali ya kwanza ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilifanyika jana usiku ambapo mashabiki wa Afrika masharik i walikuwa wakishangilia timu za nchi zao. Washiriki mahiri kutoka Cameroon,Ghana,Kenya ,Uganda na Tanzania walikutana uso kwa uso ili kushindania dola za kimarekani 250,000 na kutwaa ubigwa wa Pan-African.
Timu ya Afrika mashariki iliyoweza kufuzu kuingia nusu fainali kutoka kipindi cha kwanza ni Francis Ngigi na Kepha Kimani kutoka Kenya. Japokuwa hawakufanikiwa kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa GUINNESS lakini walifanikiwa kuingia nusu fainali. Emerand Tchouta(24) na Abdul Salam(25) kutoka Cameroon walionesha kuwa wao ni wachezaji wazuri ambapo walifanikiwa kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa. Katika hatua ya mwisho, ambapo walifanikiwa kujipatia dola za kimarekani 5,000 kuongezea walizokuwa nazo waliposhinda mwanzoni dola 1,500.
Timu zitahitaji kuwa na umoja na kujiamini ili kuweza kujiandaa kwa hatua zinazofuata. Timu moja kutoka Dar es Salaam Tanzania wataingia uwanjani wiki ijayo itakua na Daniel Msekwa(21) na Mwalimu Akida Hamad(26).
Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi alisema, “Robo fainali ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ilisisimua katika runinga ambapo Francis na Kepha walifanikiwa kuiwakilisha Afrika mashariki katika nusu fainali. Timu kutoka Kenya na Cameroon zimefuzu kuingia nusu fainali, wiki ijayo washiriki wengine watakutana ili kujua ni nani atashinda na kufuzu hatua ya nusu fainali. Nawatakia wote kila la heri”.
Timu nne zitakazo shiriki wiki ijayo kutafuta nafasi ya kuingia nafasi ya nusu fainali ni:
Watakao kuwa na jezi za bluu ni Daniel Msekwa (21) ambaye ni kichwa cha timu, na mwenzie Mwalimu
- Akida Hamad (26). Walifanikiwa kujishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya Afrika Mashariki hivyo wana nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali.
- Wenye jezi nyekundu watakuwa wakenya, kocha wa vijana Kenneth Kamau(23) na dereva Wills Ogutu (30) wote kutoka Nairobi. Ingawawa hawakufanya vizuri sana katika sehemu zilizopita lakini wanaweza kufanya vizuri wiki ijayo wakijipanga vizuri.
- Archille Stephanie na Martial Toubou kutoka Douala Cameroon watavaa jezi za kijani. Archille atajibu maswali wakati Martial ataonesha uwezo wake wa kucheza soka. Walifanikiwa kujishindaia dola 4,000 katika sehemu zilizopita.
- Jezi nyeusi watakuwa ni Dennis Nyaku(25) na Francis Nyarko(27) wote kutoka Ho Ghana ambapo walifanikiwa kujishindia dola 1,500 katika mashindano ya kitaifa. Dennis atakuwa kichwa wakati Francis atakuwa akionesha uwezo wake wa kusakata kabumbu na kuweka chini vifaa vya uchoraji.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu yako ya mkononi.
Robo fainali ya pili ya Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV kila jumatano saa 3:15 ITV na Clouds TV saa 2:15 usiku.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.
Post a Comment