UCHACHE
wa wadau na mashabiki wa bendi ya The African Stars Twanga Pepeta katika viwanja
vya Leaders Club Kinondoni, umeanza kutia hofu wadau wake, baada ya jana shoo
yao kuhudhuriwa na watu wachache, huku Salehe Kupaza akishindwa kuwapo kwenye
onyesho lao.
Kupaza
hakuja kwenye shoo hiyo ya bonanza la kila Jumapili kwa madai kuwa anaumwa,
ingawa zipo tetesi kuwa mwanamuziki huyo tegemeo kwa Twanga Pepeta ana mpango wa
kutimka mapema mwaka huu kwa ajili ya akutafuta maisha zaidi.
Vipaza
sauti vyetu vilivyotegwa vilivyo katika viwanja hivyo vilinasa mazungumzo ya
huruma kutoka kwa wadau haswa wa Twanga Pepeta, wakionyesha wasiwasi mkubwa
kutokana na mwenendo mbovu na uchache wa mashabiki wao.
“Sehemu
kama hii ilikuwa haikamatiki kutokana na watu kuwa wengi kiasi cha wengineo
kutumia kujiimarisha kiuchumi kwa kuleta biashara zao mbalimbali, lakini sasa
kuna haja ya kuangalia kwingine kwenye mwitikio wa watu.
“Si
kila anayekuja kwenye bonanza kama hili anakuja kustarehe, wengine wapo
kibiashara, sasa kama hali hii itaendelea, kuna haja wenye bendi wajipange kabla
ya mambo hayajakuwa mabaya zaidi,” alisema mdau huyo kwa masikitiko
makubwa.
Mbali
na uchache huo, lakini Handeni Kwetu haikushindwa kuwanasa wadau mahiri wa
Twanga Pepeta, wakiwamo viwanjani hapo kupata burudani, akiwamo Mathew Kawogo
ama Mathew Kiongoz, Karima Chichi Mhandeni, Engi Muro Mwanamachame, Dito Mwopao
na wengineo.
HANDENI KWETU
Post a Comment