Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wakazi 968 wa Itigi mkoani Singida wapatiwa msaada wa mahindi wenye thamani ya shilingi milioni 18.3 na shirika la Compassion International tawi la Tanzania.

 

Mkurugenzi wa kituo cha Compassion cha kanisa la Pentekoste (FPCT), Itigi,Benedict Mpuya akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa gunia 185 ya mahindi yenye thamani ya Sh.18.3 milioni kwa watu wenye upungufu wa chakula.
Sehemu ya msaada wa mahindi yakiandaliwa kwa ajili kugawanywa kwa wakazi wa mji mdogo wa Itigi wanaokabiliwa na upungufu wa chakula.
Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Itigi walionufaika na msaada wa mahindi uliotolewa na shirika la Compassion.
Mmoja wa wakazi wa mji mdogo wa Itigi, Jesca John akitoa shukurani kwa shirika la Compassion kwa kutoa msaada wa mahindi.
Wanafunzi wa kituo cha Compassion kanisa la Pentekoste kitongoji cha Tambukareli Itigi wakipata uji.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu
Shirika lisilo la kiserikali la Compassion International tawi la Tanzania limetoa msaada wa magunia 185 ya mahindi yenye thamani ya zaidi ya shilingi 18.3 milioni kwa wakazi 968 wa mji mdogo wa Itigi wilayani Manyoni, wanaokabiliwa na uhaba wa chakula.
Mkurugenzi wa kituo cha Compassion cha kituo cha kanisa la Pentekoste Itigi ,Tambukareli (FPCT), chenye namba ya usajili T.819 Benedict Mpuya, amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa mahindi hayo, uliofanyika kwenye viwanja vya kanisa la Pentekoste Itigi.
Amesema wakazi hao 968 walionufaika na chakula hicho ni wale ambao watoto wao wanasoma katika vituo vinne vinavyoendeshwa na shirika la Compassion.
Ametaja vituo hivyo vilivyonufaika na msaada huo na namba zake za usajili kwenye mabano kuwa ni kituo cha FPCT (819), Mlowa (818), kanisa Aglikan (349) na kanisa la Morovian (556).
Akifafanua zaidi, Mpuya amesema shirika hilo la Compassion limefikia uamuzi wa kutoa msaada huo wa mahindi ili kupunguza makali ya uhaba wa njaa kwa wakazi hao.
Mkurugenzi huyo amesema mbali na msaada wa mahindi, Compassion inatoa misaada kwa wanafunzi walioko kwenye vituo ikiwemo sare, madaftari, ada, michango mbalimbali, mafuta, chakula na nguo za siku kuu.
Mpuya ametumia fursa hiyo kumshukuru Mkurugemkuu wa Compassion Tanzania Joseph Mayala kwa uamuzi wake mzuri wa kutoa msaada huyo mkubwa wa mahindi kwa wazazi/walezi ambao watoto wao wanagharamiwa masomo na shirika la Compassion.
Mpuya amesema wakazi wa maeneo ya Itigi, karibu kila mwaka wanakuwa na uhaba wa chakula, kitendo kinachochangiwa na uwepo wa ukame mkali unaosababishwa na mvua chache kunyesha.
 
MO BLOG
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top