………………………………………………………………………………
WAKATI uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya kusimamia mchakato wa katiba katika Kata ukiwa unatarajiwa kufanyika Aprili 4 mwaka huu, Diwani wa Kata ya Saranga wilayani Kinondoni, Efraimu Kinyafu (Chadema), amewataka wakazi wakata hiyo kujitokeza kwa wingi katika mitaa yao, kwa ajili ya uchaguzi huo.
Akizungumza na mtandao wa Fullshangweblog jijini Dar es Salaam jana, Kinyafu alisema uchaguzi huo ni muhimu kwa kila mkazi wa kata hiyo kwa kuwa utatoa wajumbe ambao watasimamia suala zima la mchakato wa upatikanaji katiba mpya ambayo ni muhimu kwa maisha yao.
Alisema uchaguzi huo utafanyika siku moja katika mitaa yote saba ya kata hiyo kuanzia 2:00 asubuhi hivyo ni wajibu wa kila mmoja wenu kuhakikisha anatekeleza demokrasia kwa kwenda kumchagua mjumbe wanayemtaka.
Kinyafu aliitaja mitaa hiyo kuwa ni Matangini, Stop Over, Upendo, Michungwani, Kimara B, King’ong’o na Saranga, ambako maelekezo yote yatatolewa na wenyeviti wao kuhusiana na utaratibu mzima vituo vilipo.
“Nawaomba wananchi wangu wasihangaike siku hiyo kwa kwenda katika mtaa ambao si wa kwake kwani uchaguzi huo uko karibu na wao kwenye mitaa yao wanayoishi cha msingi wajitokeze kutimiza haki yao ya msingi wasikubali kuipoteza”alisema Kinyafu.
Kinyafu alisema wito wake kwa wasimamizi wa chaguzi hizo wasijaribu kuvuruga kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuvuruga zoezi zima kitendo ambacho si lengo la chaguzi hizo.
Post a Comment