WANAWAKE wawili katika
Manispaa ya Musoma maeneo tofauti wamejinyonga huku mmoja akijinyonga kwa
kutumia mkanda wa suruali na mwingine akijinyonga kwa kutumia mtandio wa nguo
yake
Katika
tukio la kwanza mwanamke aitwaye Rudia kyango umri wa miaka 40 Mkazi wa kata ya
Kigera Manispaa ya Musoma amekutwa amekufa kufuatia kujinyonga kwa kutumia
mkanda wa suruali na kuleta simanzi kubwa kwa familia yake.
Tukio hilo lilitokea
usiku wa kuamkia april 13 mwaka huu ambapo marehemu alijinyonga kwa kutumia
mkanda wa suruali na kufariki dunia na mara baada ya wakazi wa eneo hilo kufika
nyumbani kwa marehemu walitoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi kigera na
polisi kuuchukua mwili wa marehemu kwa kwaajili ya uchunguzi wa kitabibu katika
hospitali ya mkoa wa mara.
Wakati huo huo Mwanamke
mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama marwa Mkazi wa Mtaa wa
Ghandhi manispaa ya musoma anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 27 hadi 30
amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio wa nguo yake akiwa
chumbani.
Tukio hilo limetokea
asubuhi leo (jana) katika mtaa wa ghandi mjini Musoma baada ya watoto wake
kwenda shuleni ambapo majirani walimshuhudia na kutoa taarifa
polisi.
Majirani hao waliiambia
blog hii Mwanamke huyo huenda alichukua maamuzi hayo baada ya watoto wake kwenda
shuleni na kubaki pekee yake nyumbani.
wamekumbana na mama huyo
akiwa amejipiga kitanzi shingoni kwa kutumia mtandio wa nguo na kufariki
dunia.
Umati wa wakazi wa
Manispaa ya Musoma ulijaa katika eneo la tukio huku simanzi zikitawala
kufuatia kifo hicho cha kujinyonga ambapo marehemu kabla ya kifo chake alikuwa
anafanya kazi kwa mtu binafsi ya kuuza vinywaji baridi.
Jeshi la polisi
lilifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwaajili ya
uchunguzi wa kitabibu na pia kuchunguza kubaini kilichopelekea kifo cha
marehemu huyo.
Source: Shomm
Binda


Post a Comment