BIBI MWAJUMA
MPONI AKIWA HOI MARA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA MAJI
WAZEE
WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA
KUSHOTO NI SHIJA NKWABI (80) NA MWAJUMA MPONI (65).
Bibi huyo baada ya
kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza vya maduka mjini
kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala chini ya miti au chini ya
magari yaliyopaki.
Kwa mujibu wa madreva
wanaopaki magari yao eneo hilo wameiambia blog hii kuwa hata wao walishawahi
kumkosa kumgonga mara nyingi katika eneo hilo.
MATUKIO KATIKA PICHA
ASKARI WA USALAMA
BARABARANI WAKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA.
BIBI MWAJUMA AKIWA
HOI BAADA YA KUKANYANGWA NA GARI
AISEEE INASIKITISHA
SANA
MGUU WA KULIA WA
BIBI HUYO UKIWA UMEKATIKA KABISA NA KUSHIKILIWA NA NGOZI TU
VIJANA WA KAHAMA
MJINI WAKIWASADIA POLISI KUUPAKIA MWILI HUO KWENYE GARI.
BIBI MWAJUMA
AKITEREMSHWA HOSPITALINI.
HAPA VIJANA WA
KAHAMA WAKIMSUKUMA BIBI HUYO KUMUINGIZA HOSPITALINI ,TAFADHALI USINIULIZE MANESI
NA MADAKTARI WALIKUWA WAPI KUTEKELEZA JUKUMU LAO.
VIJANA WAKIENDELEA
KUJITOLEA KUMSAIDIA BIBI HUYO ILI AWAHI KUPATA MATIBABU,SWALI LANGU NI JE WANA
UZOEFU WA KUSUKUMA WAGONJWA KATIKA MAGARI HAYO?
KAHAMA
Bibi
mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwajuma Mponi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya
miaka 75 hadi 80 amefariki dunia leo baada ya kukanyagwa na gari la maji taka
wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Kwa
mujibu wa mkuu wa polisi wilayani Kahama, Gerge Simba, Bibi huyo amekanyagwa leo
mchana maeneo ya nyuma ya hospitali ya wilaya hiyo wakati akiwa amelala chini ya
gari hilo kwa ajili ya kivuli.
Simba
amesema Bi Mwajuma amefariki dunia mida ya saa moja jioni leo wakati akipatiwa
matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana majeraha makubwa
yaliyompata ikiwemo kuvunjika vibaya mguu wake wa kulia.
Hata
hivyo Simba ametoa wito kwa madereva kuwa makini na kuhakikisha wanakagua chini
magari yao sehemu wanapopaki au kupiga honi kabla ya kuondoka kwani ni hatari
kwa wazee wanaokuwa wanajizuia jua na hata kwa watu wengine.
Amesema
dereva wa gari hilo ambaye alikimbia kufuatia tukio hilo, kwa sasa anashikiliwa
na polisi kwa mahojiano baada ya kukamatwa jioni hii maeneo ya Kahama
mjini.
Kumbukumbu
zimebaini kuwa Bibi huyo ni mmoja kati ya wale walioanguka April 3 katika kata
ya Mhongolo wilayani Kahama na kupelekwa polisi kwa kudhaniwa kuwa ni
wachawi.
Bibi
huyo baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza vya
maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala chini ya miti au
chini ya magari yaliyopaki.
Credits: Kb blog
Post a Comment