Mazoezi
ya Mnyama Simba sports Club, “Taifa Kubwa” visiwani Zanzibar kujiandaa
na mechi ya watani wa jadi jumamosi uwanja wa taifa Dar es salaam
Kwa
Lalalumpa Malysia, Dar Young Africans wakijifua visiwani Zanzibar
kujiandaa kufuta fedheha ya mabao 5-0 jumamosi ya wiki hii uwanja wa
taifa
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wakati
joto la pambano la watani wa jadi Jumamosi katika uwanja wa taifa majira
ya saa 10 jioni likizidi kushika kasi zaidi katika viunga vya Dar es
salaam na maeneo yote ya Tanzania, tayari shirikisho la soka Tanzania
TFF limetangaza viingilio vya mchezo huo wa kufunga pazia la ligi kuu
Tanzania bara.
Mashabiki
watalipa Sh. 5,000 kwa lugha ya mitaani “Buku Tano” kikiwa kiingilio
cha chini zaidi katika sehemu ya viti vya Rangi ya Bluu.
Viti vya rangi ya kijani itakuwa sh. Elfu saba (7000/=), wakati viti vya rangi ya chunga itakuwa sh. Elfu kumi (1000).
Kwa wale wenye pesa zao viingilio vitakuwa ni Sh. 15,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa VIP B na Sh. 30,000 kwa VIP A.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo
alisema kuwa viingilio hivyo ni sawa na viingilio vya mchezo wa mzunguko
wa kwanza wa ligi hiyo baina ya klabu hizo Oktoba 3 mwaka jana ambapo
zilitoka sare ya 1-1.
Wambura alisema tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo, yaani Ijumaa wiki hii katika vituo mbalimbali vitakavyotajwa.
Pia
aliwataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kutazama mechi hiyo
yenye mvuto wa aina yake huku akiwatahadharisha na uwepo wa tiketi
bandia hivyo wanunue tiketi katika vituo husika.
Tayari miamba yote miwili ya soka la Tanzania ipo mafichoni visiwani Zanzibar sehemu tofuati kujiwinda na mtanange huo.
Kwa
nyakati tofauti makocha na viongozi wa timu hizo pamoja na mashabiki
wamekuwa wakitambiana huku kila mmoja akijiamini kuwa lazima apate
ushindi.
Yanga
wanakumbuka kipigo cha 5-0 msimu wa mwaka jana na kinawazunguka zaidi
vichwani na wanahitaji kulipa kisasi msimu huu ambapo tayari ni
mabingwa, wakati Simba wana hasira ya kupoteza nafasi ya ubingwa na
mshindi wa pili msimu huu.
Simba kwa sasa inawatumia vijana zaidi wakati Yanga inawatumia mafaza wote na vijana wake.
Tusubiri
nini kitatokea siku ya jumamosi uwanja taifa jijini Dar es salaam,
majira ya saa kumi kamili jioni kwa saa za Afrika Mshariki.
Yanga
wameweka kambi yao kisiwani Pemba katika hoteli ya Samail mkabala na
benki ya PBZ, wakifanya mazoezi Uwanja wa Gombani wakati Simba wameweka
kambi maeneo ya Mbweni JKT Zanzibar wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Mao Dze Tung.
Post a Comment