Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla
(katikati) akimkabidhi nahodha wa chuo kikuu cha St.John’s, Mkole
Mpangala fedha taslim Sh.500,000 baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya ‘Safari Lager Higher Learing Pool Competition 2013’ katika mkoa wa Dodoma, (wa pili kushoto), mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani wa Dodoma (DOPA),Fred Mushi.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (mwenye
suti) akifurahi pamoja na wachezaji wa chuo cha St. John’s baada ya kutwaa ubingwa wa ‘Safari Lager Higher Learing Pool Competition 2013’ Mkoa wa Dododma.
***************************
Na Mwandishi Wetu.Dodoma
CHUO
kikuu cha St.John's, juzi kilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa
mashidano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani hapa ya
'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013' baada ya kukifunga
chuo kikuu cha UDOM magoli 13-3 katika mchezo wa fainali ya mashindano
hayo.
Mashindano hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla, yalifanyikia kwenye wa Royal Village.
Jumla
ya vyuo vikuu vinne vya mkoani hapa vilishiriki mashindano hayo ambayo
yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya
Safari Lager.
Chuo
cha St. John's kwa kutwaa ubingwa huo kwa mwaka wa pili mfululizo licha
ya kujinyakuia fedha taslim Sh.500,000 pia kitauwakilisha mkoa wa
Dodoma katika fainali za taifa ambazo zitafanyika kuanzia Juni mosi
mwaka huu jijini Dar es salaam.
Fainali hizo zitashirikisha vyuo vinane ambavyo vitaibuka mabingwa kwenye mikoa yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo.
Chuo
cha UDOM kwa kushika nafasi ya pili kilizawadiwa Sh.300,000 huku chuo
cha CBE kilichoshika nafasi ya tatu kiliondoka na Sh.200,000 na chuo cha
Mipango kilipewa Sh.100,000 baada ya kushika nafasi ya nne.
Kwa
upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Juma Daniel wa chuo cha
Mipango alitwaa ubingwa huo na kujinyakulia fedha taslim Sh.150,000 na
tiketi ya kushiriki fainali za taifa na Abdallah Abdallah wa chuo cha
UDOM aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kujifunga kwa bahati mbaya alishika nafasi ya pilli na kupewa Sh.100,000.
Remi
Jackson wa chuo cha UDOM naye alifanikiwa kutetea ubingwa wake kwa
mchezaji mmoja (wanawake) na hivyo kujinyakulia Sh.100,000 na tiketi ya
kushiriki fainali za taifa za mashindano hayo na Mwanaisha Abdallah wa chuo cha CBE alipewa Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya pili.
Kabla
ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri wa Habari,VIjana,
Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla aliwapongeza wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, bia ya Safari Lager kwa kuweza kuuinua mchezo huo na kuufikisha hapa ulipofika.
Makalla pia aliwapongeza viongozi wa vyama vya mchezo huo kuanzia wilaya hadi taifa kwa ushirikiano wao ambao umeendelea kumvutia mdhamini kuendelea kuudhamini mchezo huo bila ya kurudi nyuma..
"Ni
vema mkaendeleza amani na ushirikiano mlionao sasa ili mchezo wa pool
uendelee kumvutia kila Mtanzania, kwa kweli ni mchezo mzuri ambao na
mimi nitaanza kujifunza.
Nakwa
upande wa serikali inautambua kama ilivyo michezo mingine na wizara
itaendelea kuwaunga mkono katika kuuendeleza zaidi ili siku moja uweze
kuiletea heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa,"alisema
Makalla
Post a Comment