Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman akizungumza na uongozi wa
Mkoa wa Rukwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mapema leo tarehe
16.05.2013 ambapo alizungumzia mambo kadhaa muhimu kuhusu sekta ya
mahakama nchini na umuhimu wa kuboresha amani, ulinzi na usalama katika
taifa unaokwenda sambamba na kuweka msukumo wa maendeleo nchini.
Jaji Mkuu akifafanua jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Jaji Mkuu akiongoza kikao hicho kilichojumuisha msafara wake na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo (aliyesimama) Moshi Chang’a akizungumza katika
kikao hicho. (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa –
rukwareview.blogspot.com)
Post a Comment