Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema haimzuii mwananchi, asasi au taasisi yoyote kufungua kesi
Mahakamani kupinga au kuzuia mchakato unaoendelea wa Katiba Mpya.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba ametoa ufafanuzi huo kwa baadhi ya waandishi wa habari
waliofika
ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Mei 15, 2013) kutaka
ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyotolewa na Jukwaa la Katiba jijini
Dar es Salaam jana (Jumanne, Mei 14, 2013).
Katika tamko lake, Jukwaa la Katiba lilieleza nia ya asasi yake kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania
ndani ya
siku saba ili kusimamisha mchakato wa katiba Mpya kutokana kile
ilichodai ni kasoro zinazojitokeza katika mchakato wa katiba
unaoendelea.
Ruksa kwenda Mahakamani
Hata hivyo, akiongea na baadhi ya waandishi wa habari waliofika leo ofisini kwake leo, Jaji Warioba
alisema Tume yake haina tatizo na mtu au asasi kwenda Mahakamani kwa kuwa hiyo
ni haki yao ya kikatiba.
“Nimesoma tamko lao na niseme tu halina jipya. Hii si mara ya kwanza kusikia hili (la kwenda
Jaji Warioba anayeongoza Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 2 mwaka jana.
“Mimi
nasema waende ili tujue Jukwaa haswa ni nani, kwa sababu ninafahamu ni
mkusanyiko wa asasi mbalimbali na baadhi ya asasi hizohizo zimetuletea
maombi ya kuunda Mabaraza ya Katiba ya
Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
Kuhusu
marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba amesema kuwa
ingawa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba sio jukumu la
Tume, wanafahamu kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kurekebisha sheria
hiyo kama ilivyoahidiwa.
“Hili la marekebisho ya sheria ingawa sio jukumu letu, lakini nalo sio jipya. Wote tulimsikia Waziri
Mkuu hivi
karibuni kule Bungeni akisema kuwa Serikali inaandaa marekebisho ya
Sheria hiyo yatakayowasilishwa Bungeni … sasa hawa wanataka nini?,”
alihoji Jaji Warioba.
Tume ina watu wenye weledi na uadilifu mkubwa Kuhusu, mchakato wa Katiba
kukosa uongozi madhubuti, Mwenyekiti huyo amesema kuwa Tume yake imeundwa na
watu wenye sifa, weledi na uadilifu mkubwa ambao wametokana na mapendekezo ya wadau
mbalimbali yakiwemo makundi, vyama, asasi mbalimbali za kijamii na kiraia.
“Mimi
najivunia kuongoza Tume yenye watu wenye weledi na uadilifu mkubwa na
wananchi wanalifahamu hili na kwa kweli wanatuunga mkono,” alifafanua
Jaji Warioba.
Muda wa kutolewa Rasimu ya Katiba
Katika
mahojiano hayo, Jaji Warioba pia alifafanua kuhusu muda ambao Tume yake
inatarajia kutoa Rasimu ya Katiba kwa lengo la kujadiliwa na kutolewa
maoni katika Mabaraza ya Katiba.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba,
hivi sasa Tume inaendelea kuandaa Rasimu ya Katiba na wananchi watapata muda wa
kutosha kuijadili na kutoa maoni yao.
“Mpango wa Tume ni kukamilisha kazi zake ndani ya muda uliopangwa na sheria... tutatoa Rasimu ya
Katiba katika muda ambao utatosha kuwafanya wananchi na wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba kuisoma,” alifafanua Jaji Warioba.
Jaji
Warioba pia ameelezea kushangazwa kwake na kauli za wadau mbalimbali
kuhusu utendaji kazi wa Tume na kusisitiza kuwa wananchi na wadau
wengine wasubiri Rasimu ya Katiba itolewe na
Tume ndipo watoe maoni.
“Nadhani itakua ‘fair’ (sawa), tukishatoa rasimu ndiyo watu watuhukumu,” alifafanua Mwenyekiti huyo
ambaye pia alishawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Tusiwabeze Wananchi
Kuhusu
madai kuwa wananchi waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya
Wilaya hawana uwezo na waledi wa kujadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu
ya Katiba, Jaji Warioba amesema
madai hayo hayana msingi na yanabeza maamuzi ya wananchi.
Mwenyekiti huyu ameongeza kuwa uamuzi wa Tume kushirikisha wananchi kuanzia ngazi ya mitaa, vijiji,
vitongoji na shehia ulilenga kuwapa wananchi hao fursa ya kuchaguana na
kuongeza kuwa wananchi walitumia fursa hiyo vizuri.
“Wanaosema
haya wanawabeza wananchi waliowachagua hao wajumbe,” alisema Mwenyekiti
huyo na kuongeza kuwa taarifa ambazo Tume yake imezipata zinaonyesha
kuwa katika wajumbe hao kuna
wananchi wasomi na wenye weledi wa kutosha kujadili rasimu ya katiba.
Mwisho.
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
Ohio Street,
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (00 757 500800,
Website: http://www.katiba.go.tz/
Post a Comment