UCHUNGUZI uliofanywa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), juu ya tukio la kuvamiwa na kuteswa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda umetokana na taaluma yake. Ripoti iliyotolewa jana na Katibu wa TEF, Neville Meena, imebaini hoja nne zilizosababisha madhila yaliyompata Kibanda kuwa ni kazi yake ya uandishi wa habari, uhusiano wa kisiasa na vyama au wanasiasa mbalimbali.
Taarifa hiyo pia inatilia mashaka baadhi ya mienendo ya watu akiwemo kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandao ya kijamii siku ya Machi 6, 2013.
“Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick naye alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo. Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili, fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.
“Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu wengi, hasa baada ya kueleza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kawaida mwendo wake hauwezi kuzidi dakika 10.
“Pia taarifa za uchunguzi wa timu hii zinathibitisha kuwapo kwa utata juu ya madai ya kuibwa kwa simu za Joseph Ludovick, kwani simu yake ya tigo (inayodaiwa kuibwa) ilitumika saa 01:21 asubuhi siku ya Machi 6, 2013. Muda huu ofisi za Serikali na Kampuni ya Tigo zilikuwa hazijafunguliwa,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Vile vile uchunguzi huo umebaini kuwa maisha ya wanahabari yapo hatarini na hatari hiyo inatokana na makundi mengi yenye maslahi ya kuwaona wanahabari wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa maslahi yao haramu.
Pia uchunguzi umebaini kuna hatari kubwa inayowakabili waandishi, wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa TEF, alitekwa usiku wa Jumanne ya Machi 5, 2013 akiwa katika lango la kuingia nyumbani kwake Mbezi Juu.
MTANZANIA

Post a Comment