Bi Jane Mlelwa aliyekaa
kitandani akiwa amebeba mmoja wa wawatoto watano aliowazaa kabla ya watototo
hao kufa wote(Picha na maktaba)
Hawa ndio watoto aliojifungua
katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kesho wakafaliki dunia (Picha na maktaba)
..........................................................................
Na Nathan
Mtega,Songea
MWALIMU
Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma aliyejifungua
watoto watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo Mei 25 mwaka huu
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea na watoto hao
kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla hawajafariki dunia ameruhusiwa kutoka
hospitalini hapo.
Akizungumza na Demashonews kwa njia ya
simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani kwake Ruhuwiko mjini Songea alisema alilazimika
kuomba kutoka wodini kwa sababu alikuwa akijisikia uchungu anapowaona wanawake
wenzake wodini humo wakiwakumbatia watoto wao baada ya kujifungua huku wa kwake
wote wakiwa wamefariki dunia baada ya
kuzaliwa.
Alisema kuwa muda wote
aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake kufariki huku akiwa bado anauguza
kidonda cha upasuaji aliofanyiwa alikuwa akilia muda wote anapowaona wanawake
wenzake waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo akaamua
kuomba aruhusiwe kutoka hospitalini hapo.
‘’Niliomba kuruhusiwa kutoka hospitali
na kwenda kujiuguza kidonda nyumbani kwa sababu ya uchungu na majonzi niiiyokuwa
nikiyapata wodini hapo ninapowaona wanawake wenzangu waliojifungua
wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao huku wa kwangu wakiwa
wameshazikwa”alisema Bi.Mgaya
Aidha aliushukuru
uongozi wa hospitali hiyo pamoja na wafanyakazi wote kwa namna walivyomuhudumia
yeye pamoja na watoto wake watano waliozaliwa na kuishi kwa muda wa masaa ya
kumi ambapo alisema kuwa yote yaliyotokea anaamini kuwa ni mapenzi ya
Mungu.
Mganga Mkuu mfawidhi wa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Dkt.Benedict Ngaiza akizungumza na
mwandishi wetu kwa njia ya simu kuwa waliamua kuridhia ombi la mama huyo
kuondoka hospitalini hapo baada ya kujiridhisha kuwa anaendelea vizuri kwa
sababu walifanya kila walichoweza kukoa uhai wake na watoto lakini watoto
walifariki baada ya masaa kumi.
Wakizungumza baadhi ya
wananchi waliomshuhudia mama huyo na watoto wake baada ya kuzaliwa na
kabla hawajafariki walisema kuwa kuna kila sababu kwa kila mwenye uwezo
wa kumsaidia mama huyo kwa namna yoyote afanye hivyo
Bi.Marietha Ngonyani na Lusi Haule wakazi
wa mjini Songea waliwaomba wananchi mbali mbali kujitolea kumsaidia mama huyo
kwa sababu bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa na pia tukio hilo
limemuathiri kisaikolojia pia hivyo anahitaji
faraja.
Chanzo:Demasho
Post a Comment