*Sekta ya viwanda, ulinzi, majumbani waula
*Wageni wanaofanya kazi za wazawa kudhibitiwa
Kwa mujibu wa Waziri Kabaka, nyongeza hizo za mishahara zimezingatia tija na hali ya uzalishaji na utoaji wa huduma nchini.
Alisema viwango hivyo pia vimezingatia uwezo wa waajiri na wazalishaji katika kila sekta, mfumuko wa bei na kulinda ajira nchini ili wafanyakazi wasipunguzwe kazi.
Kabaka alisema wizara yake imeendelea kuimarisha utaratibu wa ukusanyaji wa ajira na kwamba mwaka 2012/13 jumla ya ajira 27, 4030 zimepatikana.
Kabaka alisema kati ya hizo, ajira 8,603 zilitangazwa na sekta binafsi wakati ajira 56,746 zilitolewa na Serikali.
Kuhusu ajira za wageni, Kabaka alisema wizara imeandaa rasimu ya Muswada wa Sheria ya Vibali kwa ajira za wageni ambao utawasilishwa bungeni mwakani.
“Lengo la Muswada huo ni kuwa na sheria moja ya kusimamia masuala ya vibali vya ajira za wageni na hivyo kuondoa utata na migogoro katika utaratibu unaotumika sasa,” alisema.
Alisema katika mwaka huu wa fedha, wizara yake ilipokea na kushughulikia maombi ya ajira za kigeni 6,424.
Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, pamoja na mambo mengine imetaka utaratibu wa utoaji ajira kwa wageni uangaliwe upya.
Kamati hiyo ilisema kwa sasa ajira hizo zimekuwa zikitolewa kiholela hasa katika kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya.
Maoni ya kamati hiyo yalitolewa na mwenyekiti wake Jenister Mhagama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Peramiho.
“Kamati inasisitiza Serikali kuharakisha sheria ya kusimamia ajira za wageni wanaokuja kufanya kazi nchini.
“Kamati pia inaitaka Serikali kusimamia kikamilifu haki za wafanyakazi katika sekta binafsi, ikiwemo mifumo ya ajira na mafao yao.
Wizara ya Kazi na Ajira imeomba kuidhinishiwa Sh. bilioni 14.958 kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida.
MTANZANIA

SERIKALI imetangaza kuwa sekta binafsi 12 nchini, zimekubali kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wake. Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/14.
Kabaka alizitaja sekta hizo kuwa ni ujenzi, shule binafsi, nishati, viwanda na biashara, hoteli na huduma za majumbani. Nyingine ni ulinzi binafsi, madini, afya, uvuvi, usafirishaji, mawasiliano na kilimo.
Katika hotuba hiyo Kabaka alisema, mishahara katika sekta ya viwanda na biashara inaongezeka kwa asilimia 43.8, wakati hoteli na huduma za majumbani imeongezeka kwa asilimia 55.2.
Kabaka alisema mishahara katika sekta ya ulinzi binafsi imeongezeka kwa asilimia 46, madini asilimia 25.2, uvuvi na huduma za majini asilimia 21.2, usafirishaji inaongezeka kwa asilimia 49 na sekta ya kilimo asilimia 42.0.
Kabaka alisema sekta nne mpya zilizoanzishwa ambazo ni ujenzi, shule binafsi, nishati na mawasiliano nazo kima cha chini kimeongezwa.
“Viwango hivyo vipya vya kima cha chini cha mshahara, vitaanza kutumika Julai mwaka huu na vitatangazwa rasmi katika gazeti la Serikali,” alisema Kabaka.

Post a Comment