Mkurugenzi
Mkazi wa FES nchini, Rolf Paasch (Kulia)akizungumza na Makamu
Mwenyekiti wa CCM -Bara Ndugu Philip Mangula,leo katika ofisi ndogo za
CCM Lumumba. ********* |
SHIRIKA la
Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung (FES), limekipongeza na kukisifu
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuendelea kujenga utawala bora na kujenga
amani ya nchi.
Akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula,
Mkurugenzi
Mkazi wa FES nchini, Rolf Paasch, alisema shirika lake linatambua juhudi
na kazi inayofanywa na CCM katika ujenzi wa demokrasia na amani ya
Tanzania.
Kwa
Upande wake Mangula, alisema katika kuhakikisha Tanzania inatunza
kumbukumbu muhimu za kihistoria za bara la Afrika, kwa makubaliano na
nchi zingine za bara hilo zimeamua kutenga eneo maalumu wilayani
Bagamoyo kwa ajili ya ujenzi wa kijiji cha kumbukumbu hiyo.
Mangula
alimwambia mkurungenzi mkazi huyo kuwa tayari eneo hilo limeshapatikana
na kwamba mchakato wa hatua zaidi katika kuelekea ujenzi wake kwa
kushirikiana na nchi nyingine, unaendelea
Post a Comment