Miss Sinza
na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo
wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi
yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza.
Na
Mwandishi Wetu
Redds Miss
Tanzania 2012 ambaye pia ni Redds Miss Sinza, Brigitte Alfred amewataka warembo
wanaowania taji la mwaka huu la kituo cha Sinza kutomuangusha kwa kufauata
nyayo zake katika shindano lililopangwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Meeda
Club.
Brigitte
alisema hayo juzi alipotembelea warembo wanaowania taji la mwaka huu katika
kinyang’anyiro hicho kilichodhaminiwa na bia ya Redds Origional, Dodoma Wine,
Clouds Media Group, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC
Africa, Saluti5.com na Sufiani Mafoto blog.
Alisema
kuwa warembo wa kituo hicho wanakazi kubwa ya kushinda taji hilo na baadaye
Miss Kinondoni na Miss Tanzania kama yeye alivyofanya.
Alifafanua
kuwa siri kubwa ya mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani
hata yeye alifundishwa na matroni wa sasa, Mwajabu Juma na waandaaji ni wale
wale.
“Sioni
sababu ya kushindwa kufanya vyema katika mashindano haya, Redds Miss Sinza ndiyo
inatetea taji la Miss Kinondoni na Miss Tanzania pia, hivyo macho ya wadau wote
wa urembo yatakuwa kwenu na ndicho kitongoji kinachofunga mashindano ya ngazi ya
chini, mnatakiwa kujituma na kuwafanya majaji kuwa na kazi ya ziada kumpata
mshindi,” alisema Brigitte.
Alisema
kuwa wadau wa masuala ya urembo wanaangalia Sinza mwaka huu itafanya nini baada
ya mafanikio makubwa ya mwaka jana. “Sisi tumejenga msingi mkubwa na kuleta
heshima kwa wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla, nanyi mna jukumu
hilo,” alisema.
Mratibu wa
mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na
kiingilio ni sh 10,000 kwa viti vya kawaida na shs 20,000 kwa viti vya VIP.
Alisema kuwa wanakamilisha maandalizi ya burudani ya siku hiyo ambayo itakuwa ya
aina yake.
Post a Comment