Sayi alisema hayo juzi usiku wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa kujadili jinsi ya kupunguza hatari ya upatikanaji wa maji na uendelevu wa huduma hiyo.
“Upatikanaji wa maji mijini unaongezeka na unaridhisha lakini kwa vijijini bado ni tatizo ambapo wizara inahakikisha ifikapo mwaka 2014 zaidi ya vijiji 1,300 katika kila vijiji 10 vitakuwa na visima vya maji,” alisema Mhandisi Sayi.
“Wadau wa sekta binafsi kwa kushirikiana nao uzoefu na mbinu mbalimbali tunaweza kufukia malengo ya huduma ya maji kupatikana kwa wingi na kwa ufanisi,” alisema Sayi.
Naye Balozi wa Ujerumani Nchini, Klaus-Peter Brandes ambaye nchi yake kupitia Shirika la Maendeleo la (GIZ) ndio waandaaji wa mkutano huo alisema, wataendelea kujitolea kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa nchi za Ukanda wa Jangwa la Sahara unaimarika.
Alisema katika ukanda huo,Tanzania imekuwa ikionyesha jitihada za kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo hivyo kuwa mfano kwa nchi za Jangwa hilo.
Awali akiwasilisha mada, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Andrew Kaggwa alisema, watu wawili kati ya kumi duniani wanakosa huduma ya majisafi na salama.
Kaggwa alisema ndani ya miaka 10 ijayo nchi ndogo za Ukanda wa Jangwa la Sahara kutakuwa na haja ya kufanya uwekezaji kwa kila mwaka kwa kutumia dola 15-70 katika pato ili kuboresha miundombinu ya kuhifadhi huduma ya maji.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment