Na
Mwandishi wetu
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Profesa John Nkoma (pichani), amewataka
watumiaji wa simu za mkononi kuhakikisha wanazisajili zimu zao kabla ya Julai 10
mwaka huu kinyume chake zitafungwa.
Taarifa
iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Mkurugenzi huyo, ilisema,
pia Juni Mosi mwaka huu saa sita usiku laini zote za simu ambazo hazijaanza
kutumika zitafungwa na hazitaruhusiwa kutumika hadi mtumiaji atakapoisajili
laini yake mpya na watoa huduma husika.
Profesa
Nkoma alisema watumiaji wa simu hizo na wananchi wanashauriwa kuunga mkono
juhudi zinazofanyika ili kufanikisha usajili huo wa namba za simu kwa ajili ya
kudumisha na kuendeleza amani, usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya
mawasiliano na Taifa kwa ujumla.
Alisema ili
kusajili namba hizo mtumiaji anapaswa kwenda kwa mtoa huduma wake au wakala
akiwa na kitambulisho chenye picha yake, kutoa taarifa
sahihi.
Profesa
Nkoma alisema Sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta (EPOCA), ya mwaka
2010, kifungu cha 131, kimeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha
kutumika namba ya simu isiyosajiliwa.
Aliongeza
kuwa adhabu ya kosa hilo ni faini ya sh 500,000 au kifungu cha miezi mitatu
ambayo itatolewa kwa yeyote atakayekiuka sheria hiyo.
Aidha,
iwapo umesajili simu yako, mamlaka inakushauri kuthibitisha usajili huo kwa
kupiga *106#, kama wewe ni mtumiaji wa huduma zilizoko kwenye mfumo wa GSM
(Vodacom, Airtel, MIC (Tigo) na Zantel), kwa wateja wanaotumia huduma za mfumo
wa CDMA (Biol, SASATEL, TCCL Mobile na Zantel Data), watapiga namba 106 ambapo
watasikiliiza maelekezo.
“Taarifa
utakayoipata inatakiwa kutaja jina lako kama mtumiaji halali wa namba husika, na
iwapo utapata jibu tofauti, tafadhali fika kwenye ofisi ya mtoa huduma wako au
wakala wake ili kurekebisha kasoro hizo”alisema Profesa Nkoma.
Post a Comment