Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28
mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja
kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the
Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini
Marrakech.
Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya
Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa
Addis.
Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla
ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan
itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa
Addis.
Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa
kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27
mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao
2-0.
Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha
msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin
Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho
Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco,
Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro
Pazi.
Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda
Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku
hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda
Marrakech.
Source:
Michuzi
Post a Comment