Hii ndio
barabara kuu inayotoka Kilombero kuelekea lfaraka,Mahenge na Ulanga,eneo
hili limekuwa kero kubwa kwa wasafiri wanaotumia barabra hiyo,
WANANACHI
wanautumia barabara kuu ya kilombero,kuelekea maeneo ya
lfaraka,Mahenge,na Ulanga,wameilalamikia serikali ya wilaya ya kilombero
kwa kushindwa kukalabati shimo kubwa lililopo barabara kuu ya
Kilombero-lfaraka na kusababsiha adhabu kubwa kwa wananchi ambao magari
yao hukwama kwenye shimo hilo na kusababisha kulala hapo usiku kucha.
Shimo
hilo klubwa lililojaa maji kufuatia mvua zinazoendela kunyesha lipo
kwenye barabara hiyo eneo la Kidatu kilometa chache kitoka Kilombero
mjini
Baadhi ya
wananchi waliohojiwa na audifacejackson blog walidai kwamba shimo hilo
ni la muda mrefu na kwamba viongozi mbali mbali wanapita eneo hilo na
kushuhudia bila kuchukuha hatua yoyote.” Bila huyu jamaa mwenye trekta
sijua hali ingekuaje,hata hivyo jamaa huyu anafanya kazi hii kwa muda wa
mchana tu ikifika jioni anaondoka zake, jana usiku kuna abiria wa basi
moja walipofika hapa wamekwama na dereva alifanya jitohadi kulivusha
gari lake bila mafaniki nakuradhimika kulala hapa huku baadhi ya abiria
waliokuwa na watoto wadogo wakilalamika watoto zao kung’atwa na Mbu na
kupigwa na baridi usiku kucha hadi alfaji trekta lilipofika na
kulivuta basi hilo, wananchi tutavumilia lakini iko siku uvumilivu
utafika kikomo”alisema Bw Abdalaman Ismail ambaye alikuwepo eneo la
tukio alishuhudia ndugu zake wakitaabika kwenye eneo hilo.
Trekta
ambalo linafanya kazi ya kuyafuta magari yanayokwama kwenye shimo
hilo,likifuta roli huku mataili yote manne yakiwa juu kufuatia roli hilo
kuwa na mzigo mzito
Basi hili likijitoa kutumbukia kwenye shimo hilo
Wananachi wakieleke kwenye basi lao ambalo lilikwama eneo hilo kwa muda mrefu,na kufanikiwa kuvutwa na trekta hiyo
Post a Comment