Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho (katikati) akizungumza wakati kufungua warsha siku moja ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na afya kuhusu ya Maambukizi ya Ukimwi na Mahusiano ya Kingono kwa Vijana nchini ambapo
warsha hiyo imeshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo AMREF, UNICEF,
Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, TGNP,
Wizara ya Afya na nyinginezo. Kushoto ni Abdoul Coulibaly wa UNESCO na
kulia ni Mwezeshaji wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu
cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo.
Mwezeshaji
wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha
Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo akitoa mwongozo kwa washiriki wa
warsha hiyo ambapo katika majumuisho yalioamuliwa kwenye warsha
iliyofanyika leo ya kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na afya kuhusu ya Maambukizi ya Ukimwi na Mahusiano ya Kingono kwa Vijana nchini yatawasilishwa katika mkutano wa Mawaziri utakaohusisha nchi 21 za Afrika Mashariki na Kusini.
Mathias
Herman kutoka UNESCO akichambua mpango wa majukumu ya nchi za Afrika
Mashariki na Kusini na kutoa ufafanuzi wa matokeo ya utafiti wa Ripoti ya hali ya Elimu na afya kuhusu ya Maambukizi ya Ukimwi na Mahusiano ya Kingono kwa Vijana nchini ambapo
ameongeza kuwa nchi inatakiwa kujipanga kwa kusaidiwa na UNESCO pamoja
na washirika kuongoza jitihada za kitaifa ambazo zitawawezesha washirika
wakubwa ambao ni vijana kushiriki katika mikakati ya kitaifa
itakayowasidia vijana nchini kujua mtazamo wao.
Pichani ni Washirki wakifuatilia uchambuzi wa Ripoti uliokuwa ukiwasilishwa na Mathais Herman kutoka UNESCO.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Ufundi stadi Bw. Raymond Benedict (kushoto) akikata kujua kuhusu mapitio ya Ripoti ya hali ya Elimu na afya kuhusu ya Maambukizi ya Ukimwi na Mahusiano ya Kingono kwa Vijana nchini , huduma zinazotolewa na serikali na nini hatma na vijana wameelewa kwa kiwango gani.
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya siku moja ilyoandaliwa na shirika la UNESCO nchini wakichangia maoni yao.
Picha
juu na chini ni Washirki wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri
kwenye warsha ya siku moja ya ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na afya kuhusu ya Maambukizi ya Ukimwi na Mahusiano ya Kingono kwa Vijana nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho.
Post a Comment