Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ASKARI POLISI MBEYA AGONGWA NA KUFA

 
 
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Mwema

Na Esther Macha, Mbeya

ASKARI Polisi wa Kikosi cha FFU Mkoani Mbeya aitwaye G.9386 Pc Patrick(23) amefariki duniabaada ya kugongwa na gari eneo la Benki kuu Jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana , Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Bw.Diwani Athuman alisema kuwa tukio hilo limetokeajuni 23 mwaka huu.

Kamanda Diwani alisema kuwa gari na dereva asiyefahamika, liligonga gari T.741 BXU aina ya March lililokuwa limeegeshwa eneo la hilo kisha kumgonga mtembea kwa miguu askari Polisi aitwaye EX.G 9386 PC Patrick(23) na kusababisha kifo chake papo hapo.

‘’Chanzo kinachunguzwa dereva alikimbia na gari mara baada ya tukio na mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Dodoma kwa ajili ya mazishi na yeyote mwenye taarifa za alipo dereva huyo na gari atoe taarifa kwenye mamlaka husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake’’alisema.

Wakat huo huo, nyumba ya vyumba 12, mali ya Teresia Mwaijibe(40), iliungua kwa moto na kuunguza vyumba 10 vya nyumba hiyo eneo la Mlima reli mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini.Kama

Kamanda Diwani amesema kuwa moto huo ulizimwa kwa ushirikiano wa wananchi, polisi na jeshi la zima moto na hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliyotokea katika ajali hiyo ya moto.

Mwisho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top