WAZIRI MKUU PINDA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, BALOZI SEFUE |
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ameunga mkono kauli
iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kutoa kibali kwa Jeshi la
Polisi kuwapiga watu wanaokaidi amri halali. Akizungumza Dar es Salaam
jana, alisema kauli hiyo imewatoa wasiwasi Watanzania wapenda amani,
huku ikiongeza hofu kubwa kwa wahalifu wenye nia mbaya na Serikali.
Alisema baada ya Pinda kutoa kauli hiyo, Watanzania walio wengi walifarijika huku waliokuwa na malengo ya kuivuruga Serikali kulalamika kwa kutoa sababu zisizojenga umoja na mshikamano tulionao.
“Kwanza kauli hii imemfurahisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema kiasi cha kumuongezea kasi ya kusimamia zaidi usalama wa raia na mali zake.
“Sikubaliani kamwe na tuhuma zinazoelekezwa kwa Pinda na baadhi ya wachache waliokuwa na mbinu chafu, tathimini inaonyesha Watanzania wamefarijika na kuondolewa na wasiwasi.
“Nawaomba raia wote waishi kwa imani na Serikali imejiimarisha sehemu zote kuhakikisha nchi inabaki na sifa yake kuwa ni kitovu cha amani duniani,” alisema Balozi Sefue.
Hivi karibuni, Pinda, alitoa baraka kwa Jeshi la Polisi kuwapiga watu wote wanaovunja amani na utulivu wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni.
Alivitaka vyombo vya ulinzi, hasa Jeshi la Polisi kuwapiga watu watakaokaidi au kupinga amri halali zinazotolewa na vyombo hivyo.
Wakati Balozi Sefue akimpongeza Pinda, tayari Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kinaendesha kazi ya kukusanya saini za watu mbalimbali kumwajibisha.
Kituo hicho kimesema hadi sasa kimekusanya saini 1,000 za watu mbalimbali ambazo zinamtaka Pinda kufuta kauli yake aliyoitoa bungeni wiki iliyopita.
Sio LHRC peke yake bali watu wengine wamepinga kauli hiyo ya Pinda.
MTANZANIA

Post a Comment