Tunu
Kavishe, Communications Manager(centre) and Musa Kitoi Acting Consumer
Retail Director in a picture with some of the winners of the Golden
Briefcase Campaign during the 2nd Draw today
Khadija Kashoro and Anorld Shirima posed on a photo with their Golden Brifcase Gift after the 2nd Draw today, right is Tunu Kavishe Communications Manager
Khadija Kashoro and Anorld Shirima posed on a photo with their Golden Brifcase Gift after the 2nd Draw today, right is Tunu Kavishe Communications Manager
18 June, 2013
– Barclays Tanzania leo imefanya droo yake ya pili ya kampeni ya
Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase kwa wateja wake. Droo hii
inawapa fursa wateja 13 kujishindia masanduku 13 ya dhahabu kwa muda wa
miezi mitatu.
Akiongea
na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa benki, kitengo cha wateja
binafsi, Bwana Musa kitoi alisema, “ Fursa ya ushindi iko wazi kwa kila
mteja (Wateja waliopo na watarajiwa) mwenye akaunti na Barclays Bank
Tanzania. Leo tumekamilisha droo yetu ya pili na
tumewapata washindi 13. Vile vile tunatoa zawadi kwa washindi wa droo ya
kwanza iliyofanyika tarehe 22 Mei 2013, katika masanduku kumi na tatu
ya dhahabu. Kila mteja atachagua sanduku na kulifungua ili kuweza kujua
zawadi yake. Zawadi zilizopo ni i-Pad, Home theatre, Mashine za kufulia
na vocha za zawadi.
Bwana
Kitoi aliongeza na kusema kuwa “ukiweka pesa zako benki na ukawa na
salio lililokusudiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, wewe ukiwa kama mteja
wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia kwenye droo hii na
utapata nafasi ya kujinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla
atajinyakulia zawadi ya tshs millioni kumi (10,000,000 TZS)” mwisho wa
kampeni. Kampeni hii ilizinduliwa rasmi tarehe11 Aprili 2013 na
itaendelea hadi tarehe 30th June 2013.
Shindano
hili liko wazi kwa wateja binafsi, wapya na wa zamani, ambao wanaweka
fedha zao na benki yetu hapa Tanzania. Wateja ambao watatakiwa kuingia
katika promosheni hii ni wale tu wenye account ya hundi (Current
Account) au amana (Savings), na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye
account kwa shillingi laki tano za kitanzania (500,000 tzs)au zaidi, na
salio hili libakie kwenye account hadi mwisho wa mwezi bila kupungua,
Kila ongezeko la shillingi Laki tano linampatia mteja ingizo la ziada
katika katika droo ya mwezi husika..
Zawadi
kubwa ya shilling million kumi za Kitanzania (shs. 10,000,000)
itatolewa mwisho wa kampeni. Zawadi zote zitawekwa kwenye Barclays
Golden Briefcase ambapo kila mshindi atatakiwa kuchagua mojawapo kisha
kuifungua ili kujua alichojishindia. Zawadi zinazoshindaniwa kila mwezi
ni iPads 2, vocha 8 za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya
shillingi laki 2 kila mmoja (TZS200, 000), mashine za kuoshea nguo 2, na
home theatre 1.
Post a Comment