UJENZI
WA STANDI YA MABASI MAKUBWA DODOMAUKIENDELEA, UJENZI HUU UNAOFANYWA NA
MRADI WA UENDELEZAJI MIJI WA TSCP, ULIO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU –
TAMISEMI

Na Mboza Lwandiko (OWM-TAMISEMI)
Mradi
wa Uendelezaji Miji Tanzania (TSCP), ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) ambao
ulizinduliwa rasmi 2010, umedhihirisha jinsi ulivyoshamiri kwa kiwango
kikubwa. Mabadiliko makubwa yameshaanza kuonekana katika Miji 7 ambamo
Mradi huu unaendelea na shughuli zake. Mikoa hii ni; Arusha, Dodoma,
Mwanza, Mtwara, Mbeya, Tanga na Kigoma Haya yalibainishwa hivi karibuni
wakati wa Kikao cha kutathimini utekelezaji wa Tscp kilichofanyika
Dodoma Hoteli – Dodoma.
Kikao
hicho kilikusanya wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na
wawakilishi wa Halmashauri kwa kusudi la kutathimini kama Mradi huo
unaendelea vyema kufanya ipaswavyo au la. Pia kubaini kama matakwa ya
mipango ya Mradi yanafanikiwa na kutoa ushauri ambao utasaidia
kufanikisha mafanikio ya kutimiza makusudi ya Mradi kama inavyotarajiwa.
Tscp
inafadhiliwa na Benki ya Dunia na DANIDA; Jumla ya gharama zilizotolewa
ni Dola za Kimarekani Milioni 175.5, ambapo Milioni 163.2 ni kutoka
Benki ya Dunia na Milioni 12.2 ni kutoka DANIDA.
Kabla
ya Kikao cha kutathimini Tscp kwa ujula, Timu kutoka Benki ya Dunia,
DANIDA na Wawakilishi wa Tscp walitembelea shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Mradi katika Miji ya Arusha, Mwanza, Mtwara na Mbeya ili
kujionea kikamilifu yale yaliyotekelezwa katika maeneo hayo.
Wakiwa
katika Mji wa Mwanza, Mtaalam wa Mazingira wa Benki ya Dunia; Jane
Kibassa aliwataka wawakilishi wa Tscp – Mwanza kuwa makini katika
kuhakikisha usafi wa daraja na mifereji ili kuepukana na tatizo la
kuziba kwa mifereji kwa uchafu, pamoja na kuepukana na magonjwa
nyemelezi yanayosababishwa na uchafu. Vile vile mshauri wa Kimataifa wa
Tscp, Linda Skoog’s alisisitizia kutunzwa vyema kwa vifaa vya mfumo wa habari za kijiografia(GIS).
Wakati
akitoa hotuba yake katika Kikao cha Kutathimini Utekelezaji wa Tscp,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa – Mhe. Aggrey Mwanri alisema kwamba kwa ujumla kazi ya
Utekelezaji wa Tscp unaridhisha.
Kwa
upande wa Mtaalam wa Miji wa Benki ya Dunia,World, Andre Bald alihimiza
umuhimu wa kuzingatia maboresho katika maeneo yaliyoonekana kuwa na
udhaifu katika Miji yote 7. Aidha alipongeza sana Mji wa Arusha kwa
kuonekana kufanya kazi saba yake vizuri sana na kuitaka Miji mingine 6
kuiga mfano kutoka kwa Mji wa Arusha.
Kabla
ya kumalizika kwa Kikao hicho. Wafadhili na wajumbe wengine wa kikao
walitembelea shughuli mbalimbali za Mradi zilizomo Dodoma Manispaa na
CDA. Wakitembelea maeneo hayo. Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Onur Ozlu
alisema; “ Amefurahishwa na barabara zilizo na maeneo maalum ya wapiti
kwa miguu. kwakuwa ni hatari sana kwa watu kutembea katika barabara
pamoja na magari, baiskeli na pikipiki”. Naye Kaimu Katibu Katibu Mkuu,
OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini akitembelea eneo la Kisasa alisema; “
Hakuna mashaka kwamba eneo hili limekuwa na mtazamo mpya kabisa
ukilinganisha na miaka miwili tu iliyopita”.
Arusha,
Maendeleo makubwa yamejitokeza pia; Kwa barabara, msongamano wa magari
umepunguzwa, kwa marekebisho ya barabara za mijini, kwenye maeneo
yaliyofanyika karibu na eneo la biashara, ambapo barabara hizo
zilizokuwa katika hali mbaya. Sasa barabara hizo zimewekewa lami, zina
taa za barabarani na mifereji ya kudumu ya maji pembezoni mwa barabara
hizo.
Sasa
Manispaa ya Arusha imeunganisha barabara nyingine ambazo zitasaidia
kupunguza msongamano wa Magari katikati ya Mji. Barabara hizo ni pamoja
na barabara ya Majengo-Bumico (inayounganisha barabara ya Dodoma na
Arusha-Namanga, ambapo standi ya basi ya sasa, itahamishwa, na barabara
ya Col. Ndomba (itaunganisha barabara ya Njiro na Engira) na kuendeleza
ile ya Njiro.
Kwa
kigoma, shughuli ambazo zinatekelezwa na mradi, zilikuwa pamoja na;
Ujenzi wa barabara, ujenzi wa madaraja, ujenzi wa standi za mabasi na
malori na ujenzi wa dampo. Mabadiliko makubwa ya kupendeza yameonekana
zaidi kwenye standi za mabasi.
Benki
ya Dunia imechangia tena kwenye miradi mingine ya kuendeleza Miji
Tanzania, ambapo Miradi hiyo inategemewa kufanyika katika maeneo mengine
yote ambayo haikuwa na mradi wa tscp. Mradi huo unajulikana kama; The
Urban Local Government Strengthening Programme – (ULGSP).
Post a Comment