WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi ya kupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.
Taarifa iliyonaswa na
kutoka katika mitandao mbalimnali nchini Uingereza na Marekani zinaeleza
kwamba mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja nchini Tanzania kuwa kubwa pia
kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa Marekani imeshindwa kuthibitisha juu ya
suala la ulinzi na Usalama wa Rais Obama katika kipindi chote atakachokuwa
nchini Tanzania pamoja na baadhi ya nchi Barani
Afrika.
Taarifa hiyo pia
ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji maandalizi ya kutosha kwa sababu
ni msafara unaohusisha watu wengi pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo
wanyama.
Msemaji wa Ikulu ya
Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu kuangalia uwezekano wa Rais Obama
kuja Tanzania na baadaye kutembelea Senegel pamoja na Afrika Kusini ambapo
alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa mbili tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa
sana.
Katika msafara wa
Obama inatakiwa kuwe na ndege mbili za mwendo kasi, kwa ajili ya kulinda ndege
ya Rais,iwepo ndege za askari wa majini zinazotembea kwenye meli habarini, iwepo
pea maalum za magari zitakazo sushwa katika nchi zote tatu mapema kwa kutumia
ndege za jeshi kwa ajili kuimarisha ulinzi kabla ya Rais kutua katika nchi hizo"
alisema Mseaji wa Ikulu ya marekani Josh Earnest.
Nakala ya taarifa
hiyo pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani akisema kwamba pia katika
msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya kutolea matibabu katika kipindi
chote cha ziara ya Rais, lazima pia iwe na chombo maalum kwa ajili ya waandishi
mbalimbali wa habari pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kutoa
taarifa ya safari ya Rais ,pamoja ndege zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali
ya usalama katika hoteli zote atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara
wake.
Taarifa hiyo
ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko aliyowahi kuifanya
Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa
Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa itachukua kati ya dola za marekani
60 million sawa na tsh bilioni 96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh
bilioni 160,000,000,000.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/06/breaking-newzz-rais-obama-ahairisha.html#ixzz2WDX51uF2
Post a Comment