Loading...
Home »
Unlabelled »
HABARI ZAIDI JUU YA MTOTO ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA
Mtoto wa
miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya
kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne. Andrew Palismwe,
anayetokea Caprivi, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji
uliochukua masaa tisa kuondoa miguu miwili kwenye Hospitali ya watoto ya Red
Cross War Memorial iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini. Mtoto huyo
sasa anaendelea kupata nafuu kwenye Hospitali ya Windhoek Central nchini
Namibia, imeripotiwa. Alizaliwa akiwa na miguu miwili ya ziada chini ya tumbo
lake Aprili 6. Hali hiyo inadhaniwa kuwa ni matokeo ya mapacha ambao
hawakukamilika.
Daktari wa Hospitali
ya Windhoek Central, Clarissa Pieper alisema: "Hii ni hali ambayo mapacha
wameungana pamoja na kufuatia mimba ya mapacha ambayo hawakutengana kabisa,
lakini kuunda watoto wawili wanaokua ndani ya kila mmoja. Katika suala hili,
mtoto mwingine hauendelea kikamilifu."
Mama wa Andrew, Ruthy Mutanimiye alisema katika
hospitali hiyo kwamba mtoto wake huyo wa kiume 'amepata nafuu haraka mara baada
ya matibabu' baada ya siku nzima ndani ya chumba cha wagonjwa
mahututi.
Pia alizungumzia kuhusu
faraja yake kwamba mtoto wake alifanyiwa upasuaji ambao asingeweza kumudu
gharama zake. Serikali ya Namibia ililipia
gharama za upasuaji huo kupitia mfumo ambao husaidia wagonjwa wenye hali mbaya
wasioweza kumudu gharama za hospitali binafsi. Ester Paulus,
msemaji wa Wizara ya Afya ya Namibia na Huduma za Jamii, alisema: "Mfuko huo
ulianzishwa kusaidia wagoniwa ambao hawana njia yoyote kupata matibabu kwenye
hospitali binafsi.
"Tunashughulikia kila ombi kwa uharaka, na kwa sasa,
hakuna fomu zozote za maombi zinayosubiri kufanyiwa kazi." Alikataa
kutaja gharama za upasuaji wa Andrew, akisema: "Hakuna kiasi cha pesa
kinachoweza kulinganishwa katika uokoaji maisha."
on Friday, June 21, 2013
Post a Comment