Hivi ndivyo Ndege ya Air Force One ambayo inatumiwa na Rais Barack Obama
itakavyokuwa ikisindikizwa na kupewa ulinzi na Ndege Ya Kivita ya
Marekani Pindi atakapokuwa akija Jijini Dar mnamo mwezi wa saba.
Wajuzi
wa Mambo wanasema Kuwa Raisi Obama Amekuwa na Ulinzi Mkubwa Sana
tofauti na maraisi wengine wa Marekani. Katika Hali isiyo ya Kawaida kwa
NChi ya Tanzania Ndege za Kijeshi kutoka Jeshi la Marekani Zitakuwa
Zikirandaranda Kwenye Anga ya Tanzania Anga ambayo inaitwa Anga ya Raisi
yote ni Katika Kuimarisha Ulinzi kabla na wakati Raisi wa Marekani
Barack Obama Atapokuwa akiwasili na kuwepo Nchini Tanzania
Inasemekana
Raisi Obama atakuwa na Convoy ya Askari wapatao zaidi ya 1600 ambao
wengi wao watawasili kabla ya yeye kufika Nchini Tanzania Kwaajili ya
Kuimarisha Ulinzi
Post a Comment