NA DUSTAN SHEKIDELE,
MOROGORO
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja jana usiku alinusurika kifo baada ya kugonga nyumba wakati akijifunza kuendesha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 952 BTJ.
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja jana usiku alinusurika kifo baada ya kugonga nyumba wakati akijifunza kuendesha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 952 BTJ.
Tukio hilo lilitokea majira
ya saa tatu usiku maeneo ya uwanja wa ndege jirani na Chuo cha Ujenzi njia panda
ya kuelekea gereji ya Msuya.
Mbali na mwanamke huyo
kunusurika kifo, pia familia iliyokuwa ikiishi kwenye nyumba iliyogongwa nayo
ilinusurika baada ya gari hilo kuvunja ukuta wa nyumba na kuingia mpaka chumbani
ambako familia ilikuwa inajianda kulala.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mtandao huu walidai kwamba mwanamke huyo ambaye bado hajaiva kwenye udereva alikata kona iliyo eneo hilo kwa mwendo kasi.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mtandao huu walidai kwamba mwanamke huyo ambaye bado hajaiva kwenye udereva alikata kona iliyo eneo hilo kwa mwendo kasi.
"Huyu mama anajifunza kama
unavyoona kibao cha 'L' kwenye gari yake, uzembe alioufanya alikata kona hii kwa
mwendo wa kasi na kwamba badala ya kukanyaga breki alikanyaga moto na kuzidisha
kasi ndipo alipogonga nyumba hii." Alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa
jina la Jumanne Athuman.
habari na picha kwa hisani
ya GLOBAL PUBLISHER
Post a Comment