Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe akitoa hiotuba bungeni.
*********
Japan itatoa msaada wa takriban dola billion moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa maendeleo ya kiuchumi na juhudi za kibinadamu, kadhalika usalama na hatua za kupambana na ugaidi, huko kaskazini mwa Afrika.
Japan itatoa msaada wa takriban dola billion moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa maendeleo ya kiuchumi na juhudi za kibinadamu, kadhalika usalama na hatua za kupambana na ugaidi, huko kaskazini mwa Afrika.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, alitangaza kuhusu msaada huo Jumapili, ikiwa ni siku ya pili ya mkutano wa siku tatu wa kimataifa wa Tokyo, juu ya maendeleo ya Afrika, unaofanyika huko Yokohama, kusini mwa mji mkuu.
Fedha hizo ni sehemu ya msaada wa dola billion 32, kwa sekta za serikali na za kibinafsi, alisema Bw. Abe.
Anasema uwekezaji wa fedha za umma na za kibinafsi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, unalenga kusaidia ukuaji wa bara hilo na kushawishi mashirika ya Japan kuwekeza huko.
Waziri mkuu huyo alianza kulilenga bara la Afrika kwa nafasi za uwekezaji, muda mfupi baada ya kuchukuwa mamlaka mwaka jana.
Takriban viongozi 50 wa kiafarika wako nchini Japan kwa mkutano huo, utakaojadili masuala ya kiuchumi na maendeleo na kadhalika wasiwasi juu ya amani na usalama katika eneo hilo. Mkutano huo unaofanyika kila miaka mitano, ulianza hapo mwaka 1993. Mkutano huo unatarajiwa kumalizika Jumatatu. Chanzo: voaswahili
Post a Comment