Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .
Akizungumza ofisini
kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu
kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani
kutaharibu upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali kwenye viwanja
hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya
tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..
Hata hivyo viongozi wa
chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na kuanza kujikusanya
uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali
iliyoleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi
hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja
alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo
ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu
waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha
Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya
dakika kadhaa mabumu yalianza kusikika.
Baadhi ya viongozi wa
juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John
Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee...
Post a Comment