NAPE NNAUYE.GODBLESS LEMA.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe.
JESHI la Polisi limetishia
kuwakamata Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema na limesema litamhoji Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya
wanasiasa hao kudai kufahamu watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini
Arusha jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja aliwataka
wanasiasa hao kuwasilisha ushahidi wa kile wanachofahamu kuhusu kulipuliwa kwa
bomu hilo.
Juzi, Mbowe akiwa na Lema, alisema wana
ush
ahidi wa picha za video zikiwahusisha polisi na kulipuliwa kwa bomu hilo
katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani kwa
Chadema, Jumamosi iliyopita.
Mkwara wa Chagonja
Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na
Lema kupeleka ushahidi ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.
“Tunamtaka Mbowe na Lema kutoa ushahidi
wa askari wetu kuhusika na tukio la bomu pale Soweto. Wasipofanya hivyo
tutatumia sheria kuwalazimisha kufanya hivyo kwani yeyote mwenye ushahidi
unaoweza kusaidia upelelezi wa kosa la jinai akikataa kuuwasilisha kwa vyombo
husika anaweza kuchukuliwa hatua,” alisema.
Nape naye kuhojiwa
Kwa upande wake, polisi limesema
litamhoji Nape ambaye alikaririwa jana akidai kuwa Chadema ndiyo waliohusika na
urushaji wa bomu kwenye mkutano wao baada ya kuhisi kushindwa kwenye uchaguzi
wa kata nne za Jiji la Arusha.
Kamishna Chagonja alisema watamhoji ili
kusaidia kazi yao ya upelelezi. Nape aliihusisha Chadema kwa kauli alizoita za
kutishia amani zilizowahi kutolewa siku za nyuma kabla ya uchaguzi wa kata za
Arusha.
Watatu wakamatwa
Kamishna Chagonja alisema watu watatu
wamekamatwa wakihusishwa na tukio la kulipuliwa kwa bomu mkoani Arusha.
Alisema watuhumiwa hao wanahojiwa na polisi
na watafikishwa mahakamani muda wowote ushahidi wa kutosha utakapopatikana au
kuachiwa huru wakigundulika kutokuhusika.
Post a Comment