Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI TANAPA CHAHITIMU MAFUNZO RUAHA NATION PARK

 


 1Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya Ruaha kandokando ya mto Ruaha wakipewa mafunzo hayo na wakufunzi Martin Mthembu kutoka taasisi ya African Field Rager Training Services ya Afrika kusini, kikosi hicho maalum cha TANAPA kilikuwa na askari 20 wamehitimu mafunzo hayo askari 19 moja hakufanikiwa kumaliza mafunzo kwa sababu za kiafya, Kivutio kilikuwa kwa askari mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia ameza kufanya mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu kutoka Afrika Kusini na akampa sifa na pongezi nyingi kwa uwezo wake kama mwanamke.  3Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akirejea meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo hayo 4Kikosi hicho kikitembea kusonga mbele tayari kwa kutoa heshimza zao kwa mgeni rasmi. 6 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akipokea heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya kukabiliana na ujangili katika hifadhi za taifa kulia ni Adam Swai Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Iringa na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki. 7Askari wahitimu wa kikosi hicho kushoto ni Frank Anthon Malema na Mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 8Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo 10Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Frank Anthon Malema kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 11Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Elisamehe Elisafi Mdeme kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 12Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimpongeza John Kijazi baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo 13Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.14Martin Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa maelezo kwa Allan Kijazi Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha Nation Park. 15Askari maalum wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakionyesha moja ya kazi zao wakati wakitafuta majangili katika hifadhi hizo 16Mmoja wa Askari wa kikosi hicho akilenga shabaha 17Mkufunzi wa Mafunzo hayo Martin Mthembu akielezea mafanikio ya kikosi hicho katika kulenga shabaha kwa mkurugenzi wa hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi wa pili kutoka kushoto wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Martin Loiboki na wa kwanza kushoto ni Dr. Christopher Timbuka Mhifadhi Mkuu Ruaha Nation Park 20Mkufunzi Martin Mthembu akielezea jinsi askari hao wanavyotakiwa kuwatafuta majangili huku wakiwa na maamuzi ya haraka bila kuchelewa na kutoua jangili ambaye hana madhara askari wa anatakiwa kufanya kazi yake kwa ufanisi lakini pia kulinda usalama wake yaani fanya kazi yako lakini rudi salama 21Askari mwanamke pekee Aikande Lema akilenga shabaha huku mkufunzi huyo akiangalia 22Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi naye akimshuhudia askari huyo 23Askari Aikande Lema akirejea mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na mwalimu wake kwa mafanikio katika kulenga shabaha. 24Mto ruaha 25Mnyama tembo yuko hatarini kutoweka kutokana na majangili kuwauwa kwa wingi wakichukua pembe zake 
 27 
Twiga ni mojawapo ya wanyama ambao pia wanauliwa na majangili 28Mhifadhi wa Ruaha Nation Park Paul Banga akitoa maelekezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kabla ya kuingia mbugani jana kwa lengo la kujifunza utalii wa ndani na kujionea wanyama mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi hiyo 29Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika geti la kuingilia kwenye mbuga ya Ruaha Nation Park.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUAHA NATION PARK
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top