Mjumbe wa Kamati
ya Mapinduzi Cup ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo Dr. Ali Mwinyikai akifafanua Mikakati iliyojipangia
Kamati hiyo katika kutafuta fedha za kufanikisha mashindano ya Mapinduzi
Cup.Moja
kati ya mikakati hiyo ni kuhakikisha uwanja wa michezo wa Amani
unawekewa nyasi bandia ili kuuwezesha uwanja huo kuhimili mashindano
hayo.
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Mapinduzi Cup Sharifa Khamis akielezea hatua inazoendelea
kuchukuwa Kamati yake katika maandalizi ya mashindano hayo ambayo mara
hii yanatarajiwa kuwa ya Kimataifa.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiipongeza Kamati ya Mapinduzi
Cup aliyokutana nayo kuangalia hatua wanazochukuwa katika maandalizi ya
Mashindano ya kombe hilo ambapo maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi
zinafikia nusu Karne {Miaka 50}.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
--
Timu
zipatazo 13 za Mchezo wa Soka za Kitaifa na Kimataifa zinatarajiwa
kushiriki katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa
kufanyika ndani ya kipindi cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar ya mwaka 2014.
Hayo yamejiri wakati Uongozi wa Kamati ya Mapinduzi Cup ulipokutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kumpatia taarifa kufuatia hatua
za awali za maandilizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa ya
Kimataifa.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sharifa Khamis alimueleza Balozi Seif kwamba
Kamati hiyo imezingatia agizo la Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohd Sheni la
kuzialika pia kwenye mashindano hayo Timu za Soka za China, Vuietnam na
Oman kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya Zanzibar na Nchi hizo.
Sharifa
alizitaja baadhi ya timu nyengine zitakazoalikwa katika mashindano hayo
kuwa ni pamoja na Yanga, Simba na Azam za Tanzania Bara, Tasker ya
Kenya, URA ya Uganda, APR ya Rwanda na wenyeji wa mashindano hayo timu
za KMKM,Jamuhuri na Chuoni.
“
Kamati yetu imeamua kuanza mapema maandalizi hayo kutokana na umuhimu
wa sherehe zenyewe na kikao chetu cha kwanza tumefikia hatua za
kufikiria njia za kupata fedha za maandalizi pamoja na timu
tutakazozialika kushiriki mashindano hayo “. Alifafanua Sharifa Khamis.
Alieleza
kwamba mashindano hayo yanatarajiwa kupangwa katika mfumo wa makundi
mawili Unguja na Pemba ili kuwapa fursa wapenzi wa michezo kisiwani
pemba kuona mashindano hayo.
Naye mjumbe
wa Kamati hiyo ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni,
Utalii na Michezo Dr. Ali Mwinyikai alisema Kamati hiyo pia imefikiria
kushirikisha michezo ya Pete pamoja na Riadha ili kuongeza vugu vugu la
mashindano hayo.
Dr.
Mwinyikai alieleza kwamba Kamati hiyo imeanza hatua za kuwasiliana na
baadhi ya wadau wa michezo ndani na nje ya Nchi katika hatua ya kuona
mashindano hayo yanafanyika kwa mafanikio makubwa kulingana na
maadhimisho yenyewe.
Katika
kukifanyia maandalizi ya mapema kiwanja cha michezo cha Amani Mwinyikai
alisema Kamati hiyo kwa kushirikiana na Wizara inayosimamia michezo
Zanzibar wamefikiria kukiwekea nyasi bandia kiwanja hicho ili kiwahi
kutumika katika mashindano hayo ya Mapinduzi Cup.
Alisema Wizara
ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo imeweka kifungu maalum
kitakachounga mkono kazi hiyo ndani ya makadirio ya Mapato na Matumizi
yake kwa mwaka wa fedha endapo kitapita katika kikao cha baraza
kinaoendelea.
Akitoa
shukrani zake kwa hatua iliyofikiwa na Kamati hiyo kwa kuanza vizuri
maandalizi hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na yeye binafsi itajitahidi kuunga mkono Kamati hiyo ili ifikie lengo iliyojipangia.
Balozi
Seif aliihakikishia Kamati hiyo kwamba atachukuwa jitihada za ziada
katika kuona wale wadau, Mashirika na hata Taasisi zinazofikiriwa kuunga
mkono harakati hizo kimawazo na hata uwezeshaji wanasaidia.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhimiza Uongozi wa Kamati hiyo ya
Mapinduzi Cup kuendelea na maandalizi katika hatua kubwa na makini ili
kuona lile kusudio la kufanikisha mashindano hayo muhimu linafikiwa.
“
Katika kulipa nguvu za himizo la ziada suala hili nitakuombeni kwa
hatua zinavyosonga mbele ni vyema tukakutana tena mwishoni mwa mwezi wa
Julai ili kuangalia tumefikia hatua ipi na tumekwama wapi katika Maandalizi hayo “. Aliagiza Balozi Seif.
Mashindano
ya Kombe la Mapinduzi yanayofanyika mnamo Mwezi wa Januari kila mwaka
mara hii fainali yake imepangwa kufanyika siku ya Pili ya Maashimisho ya
Sherehe za Mapinduzi Januari 12 ambayo itakuwa Tarehe 13 Januari 2014.
Uamuzi
huo umechukuliwa na Kamati hiyo ili kuwapa nafasi nzuri Wananchi na
wapenzi wa Michezo na sanaa kushiriki katika matukio yote yanayoambatana
na sherehe hizo ikiwemo burdani na muziki wa Taarabu uliozoeleka
kufanyika usiku wa kilele cha sherehe hizo.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Post a Comment