Mtuhumiwa akiwa ndani ya chumba cha mganga na Mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa kufanya mambo ya kishirikina.
Mama mmoja pichani juu ajulilikanae kwa jina la Magreth Simon Nkwera, amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la kutaka kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko kibaha maili moja mkoani Pwani na hivi sasa yupo katika kituo cha polisi Maili moja akisubiri kupandishwa kizimbani.
Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa akiwa na huyo Mganga wa Kienyeji.
Mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wa shirika la Nyumbu kibaha mkoani Pwani,akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa Shirima,Afisa polisi jeshi daraja la Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa sangoma.Habari hii imetolewa na mwenyekiti wa ukoo wa shirima bwana Godilisten Hendrick Shirima.
Post a Comment