MWENYEKITI wa CHADEMA Freeman Mbowe,
amevituhumu vyombo vya dola kuwa vinawafahamu watu walioshiriki kwenye mlipuko
wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama
hicho.
![Photo: Mbowe afichua mazito
ASEMA SMG, BASTOLA ZILITUMIKA ARUSHA
MWENYEKITI wa CHADEMA Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa vinawafahamu watu walioshiriki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama hicho.
Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.
Soma zaidi - http://swahilivilla.blogspot.com/2013/06/mbowe-afichua-mazito.html](https://fbcdn-sphotos-g-a.akamaihd.net/hphotos-ak-frc3/p480x480/996186_10152909639290247_1473666877_n.jpg)
Mwenyekiti wa
CHADEMA Freeman Mbowe
Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.
Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.
Wakati Mbowe akitoa tuhuma hizo kwa vyombo vya
dola, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu itakayoongozwa na
makamishna wawili (Paul Chagonja na Isaya Mungulu), kwenda mkoani Arusha
kuongeza nguvu ya uchunguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani
hapa, Mbowe alisema uchunguzi wa awali walioufanya wamebaini tukio hilo ni la
kisiasa na lilipangwa.
Alisema ni vema serikali ikatangaza kuachana na
mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika mikutano ya vyama
vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa watawala.
Aliongeza kuwa uchunguzi wa awali katika eneo
la tukio umebaini bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la
kutengenezwa.
Alisema katika eneo la tukio maganda ya risasi
kutoka katika bunduki ya SMG na bastola yalikutwa hali inayowafanya waamini kuna
watu waliamua kufanya tukio hilo kwa kupanga.
Mbowe alisema risasi hizo pia ni miongoni mwa
zilizopigwa kwenye tanki la mafuta la gari la matangazo la CHADEMA ambapo
zililitoboa.
Alibainisha kuwa inavyoonekana wahusika
walitaka kuzalisha mlipuko mwingine mkubwa na kuleta maafa makubwa katika
mkutano huo.
“Haihitaji uchunguzi wa kwenda mwezini katika
suala hili, ni wazi walipanga kutuua lakini wakaua watu wasiohusika. Waliouawa
hawakuwa katika mpango wao na wamekuwa wahanga kwa niaba yetu.
“Hata kama utaamua kumuua Mbowe au (Godbless)
Lema, huwezi kuiua CHADEMA kwani chama kitabaki, na wanachama wengine
wataendeleza harakati za chama kama kawaida,” alisema.
Wabunge kutohudhuria Bunge
Mbowe alisema kutokana na tukio hilo ambalo
limeua watu zaidi ya watatu, CHADEMA imeamua kulifanya ni la kitaifa na wabunge
wake watashiriki kwenye maombolezo.
Alisema kuanzia leo wabunge wote wa CHADEMA
hawatahudhuria vikao vya Bunge na watajumuika mkoani Arusha hadi misiba yote
itakapomalizika.
Alisema wanatarajia kufunga mahema katika eneo
la tukio na marehemu wote wataagwa katika eneo hilo ambapo ibada zote za
Kiislamu na Kikristu zitafanyikia hapo.
IGP aunda timu
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwema ameunda
timu ya kuongeza nguvu ya uchunguzi itakayoongozwa na makamishna wawili ambao ni
Paul Chagonja kutoka idara ya operesheni na Isaya Mngulu kutoka ofisi ya
upelelezi makao makuu.
IGP Mwema alisema baada ya tukio hilo, jeshi
hilo lilituma makamishna wawili kutoka makao makuu kwa ajili ya kuongeza nguvu
ya uchunguzi wa tukio hilo na kwamba wameshaanza kukusanya taarifa mbalimbali
zitakazoweza kusaidia kuwabaini watu waliohusika.
Alisema wameunganisha nguvu na vyombo vingine
vya ulinzi na watawasaka wahalifu hao pamoja na walio nyuma yao kwa kile
alichoeleza tukio hilo linaashiria kushamiri kwa matendo ya kigaidi
nchini.
Akizungumzia tuhuma zinazotolewa na wananchi
juu ya Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu kwa risasi za moto, IGP Mwema alisema
kila taarifa inafanyiwa kazi kwa umakini na kwamba baada ya uchunguzi watatoa
taarifa kamili kwa umma juu ya kilichotokea jijini Arusha.
Aliwaomba wananchi wenye taarifa za kuweza
kumtambua aliyerusha bomu pamoja na watu walio nyuma yake wajitokeze au wamtumie
ujumbe kupitia simu yake ya mkononi namba 0754 78 55 57 na kwamba uhusika wao
utafanywa kuwa siri.
IGP Mwema pia alisema watachunguza kauli ya
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Mwigulu Nchemba
aliyowaambia wakazi wa Kimandolu kuwa wasipoichagua CCM katika uchaguzi wa
madiwani wa Jiji la Arusha ulioahirishwa jana, watakufa.
Mwema alisema watachunguza kauli hiyo baada ya
kuulizwa swali la hatua zilichochukuliwa kabla na baada ya mlipuko huo dhidi ya
kauli ya Nchemba.
Juzi katika mkutano wa kufunga kampeni za
udiwani kwa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, kitu kinachodhaniwa
ni bomu kilipuka na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.
Chanzo: Tanzania
Daima
Post a Comment