Mkuu
wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akiongea kwa msisitizo ofisi juu ya mgogoro
ulijitokeza baina ya wachinja ng'ombe na wauzaji hapani
ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
Aliyenyoosha kidole ni Issa Bakari akionyesha banda
lililobomolewa na Afisa mifugo wa manispaa ya Songea
Hawa ni wachinjaji wa ng'ombe wakiwemo wauzaji wa
ng'ombe wakiwa katika hali ya majonzi baada ya kuvunjiwa banda la kuhifadhia
ng'ombe kabla ya kuchinja
Waandishi wa habari wakimuoji Afisa mifugo mkoa wa Ruvuma Bw. Mwaiganju aliyesimama katikati ni mwandishi wa habari wa ITV Bw. Nathan Mtega , anaefuata ni mwandishi wa habari wa radio Jogoo Millan na alieshikilia kamera ni Demasho
Waandishi wa habari wakimuoji Afisa mifugo mkoa wa Ruvuma Bw. Mwaiganju aliyesimama katikati ni mwandishi wa habari wa ITV Bw. Nathan Mtega , anaefuata ni mwandishi wa habari wa radio Jogoo Millan na alieshikilia kamera ni Demasho
Hawa ni baadhi ya ng'ombe ambao wapo uwanjani baada ya
kuvunjwa banda
..........................................................
MGOGORO umeibuka baina ya wachinjaji na wauzaji wa
ng’ombe wa Manispaa ya Songea dhidi ya baadhi ya watumishi wa idara ya mifugo wa
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao umesababisha wachinjaji na wauzaji wa
ng’ombe kuitisha mgomo usio na muda maalumu mpaka ufumbuzi
wa tatizo hilo ambalo walidai ni la muda mrefu
upatikane.
Mgogoro huo ambao ulianza Juni 4 mwaka huu majira ya
saa 12.30 jioni na kudumu mpaka majira ya saa 2 usiku mwenyekiti wa umoja wa
wachinjaji wa ng’ombe wa Mmkoa wa Ruvuma Salum
Mfamaji ambaye pia ni diwani wa kata ya Misufini alipotangaza
kusitisha huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo lilikuwa
liliwataka wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe kuondoka katika eneo hilo na kwenda
kufanyia shughuli zao katika kata ya Tanga ambako wao walidai
hakujaandaaliwa.
Akizungumza kwa niaba ya wachinjaji Issa
Bakari alisema kuwa wao kama wachinjaji hawajakaidi uamuzi wa Manispaa ya Songea
kuhamia katika eneo hilo jipya lakini walishaomba eneo hilo lifanyiwe
marekebisho muhimu ikiw ni pamoja na kuweka miundo mbinu muhimu
ikiwemo vyoo na maji kwa ajili ya usalama wa kiafya kwao na watu
wengine watakaokwenda katika eneo hilo kwa ajili ya kupata huduma
hiyo muhimu.
Alisema kuwa tangu kulipotokea mabadiliko
ya watumishi katikas halmashauri ya Manispaa ya Songea na hasa katika idara ya
mifugo kumeibuka na vitendo vya unyanyasaji kwa wachinjaji vinavyofanywa na
baadhi ya watumishi wa idara hiyo ikiwa ni pamoja na kitendo cha kuamua kuvunja
zizi la kuwafadhi ng’ombe kabla ya kuchinjwa kitendo ambacho kimefanywa bila
kutolewa taarifa kwa wachinjaji na wao wameamua kusitisha huduma hiyo kwa
jamii.
Baada ya mjadala wa muda mrefu diwani wa
kata Msamala eneo ambalo machinjio yapo Sharif Mgwasa alipowaomba
wachinjaji hao kuendelea kutoa huduma hiyo muhimu kwa jamii wakati uongozi
ukiendelea na mazungumzo ya kutafua ufumbuzi wa tatizo hilo lililojitokeza ikiwa
ni pamoja na kujua aliyeamuru kuvunjwa kwa zizi hilo bila kuzingatia utaratibu
wa ushirikishwaji wa wachinjaji’wauzaji na uongozi wa Manispaa
hiyo.
Hata hivyo wachinjaji hao waliendeleakusisitiza kuwa
hawako tayari kuendelea na huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo
utakapopatikana hali iliyoendelea mpaka Juni 4 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi
walipoamua kuanza kuchinja ingawa ni ng’ombe wachache waliochinjwa kwa sababu ya
sintofahamu hiyo iliyotokea huku eneo hilo la machinjio likitawaliwa na vurugu
zilizosababisha askari polisi kufika eneo hilo na kutuliza ghasia
hizo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph
Mkirikiti akizungumzia hali hiyo iliyojitokeza alisema kuwa hiyo imetokana na
kutokwepo kwa ushirikishwaji wa pande zote zinazohusikia lakini pia suala la
kuvunja zizi hilo haliafiki ni si utaratibu wa busara kwa sababu ni kitendo cha
kihuni na hakipaswi kufumbiwa macho kwa sababu wachinjaji na wafugaji walipaswa
kuandaliwa mazingira mapya ya kufanyia shughuli zao na suala la kuwahamisha
lingefuata.
Hata hivyo ufumbuzi wa sintofahamu hiyo unatarajiwa
kufikiwa kesho kwa kuzikutanisha pande zote kwenye ofisi ya Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Songea
credits: Demasho
Post a Comment