Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, akisikiliza kwa
makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sacoma group, Bwana. Sam
Ochieng, namna ambavyo bidhaa za Matunda na Mboga mboga kutoka nchini
Kenya zinavyopakiwa, kusafirishwa na hatimaye kuuzwa kwenye soko la
Spitfield nchini Uingereza, kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma. Umoja huo wa
Sacoma wenye lengo la kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wa africa ya
Mashariki. Mheshimiwa Waziri Mkuu, alifanya ziara kwenye Soko la
Spitafields, lililopo Stratford nchini Uingereza, kwa lengo la kujionea
shughuli za Jumuiya ya Sacoma inavyoendesha shughuli zake kwenye soko
hilo na jinsi ambavyo Jumuiya hiyo imeweza kuwasaidia Wakulima wa
Matunda na Mboga kutoka nchini Kenya, kupata soko la kuuza Bidhaa zao
hapa nchini Uingereza.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, akiangalia na kupata maelezo ya Ubora wa bidhaa unaotakiwa
kupata soko nchini Uingereza. Pichani, mstari wa pili, (kwanza
kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Ungereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe,
kwanza (kulia) ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania,
Uingereza Bwana Yusuf Kashangwa, maofisa wa Ubalozi na Viongozi kutoka
Tanzania ambao wameambatana na Waziri Mkuu nchini Uingereza kwenye
Mkutano unaofanyika leo ambao unahusu jinsi ya kutokomeza njaa na
umuhimu wa Lishe bora kwa Mama na Watoto Duniani (Hunger and Nutrition).
Mkutano huo ambao umeandaliwa na Asasi za kiserikali na zisizo za
Kiserikali, unakutanisha nchi kubwa Duniani, zijulikanazo kama G8,
Wadhamini, Wachangiaji na Watoa misaada kwenye Asasi hizo, zenye lengo
la kutokomeza njaa duniani na kusaidia kuwapatia Wamama na Watoto Lishe
bora.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe na Mkurugenzi wa Kituo cha
Biashara cha Tanzania, kilichopo London, Bwana Yusuf Kashangwa,
wakiangalia bidhaa mbalimbali kutoka nchini Kenya na kupeana ushari
jinsi gani ambavyo wanaweza kuwasaidia Wakulima na Wafanyabiashara wa
Tanzania kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma, kuweza kuuza Bidhaa zao nchini
Uingereza.


Post a Comment