NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Timu 19 zitakazoshiriki Meya's Cup2013 tayari
zimekwisha kabidhiwa vifaa vya michezo kuweza kushiriki michuano hiyo kwa mwaka
huu.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa makapteni wa timu zote
shiriki pamoja na waamuziwa michuano hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo
tarehe 15 mwezi huu (juni) 2013, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo
amesisitiza nidhamu mchezoni na kuwataka vijana washiriki kujibidiisha kuusaka
ushindi ili wajinyakulie zawadi ambazo zimenuia kusaidia kuboresha mitaji yao
sambamba na kuwaandaa kuifanya michezo kuwa sehemu ya
ujasiliamali.
Kila timu imekabidhiwa jezi seti moja ikiwa na soksi
zake pamoja na mpira mmoja kwa kila timu nazo zawadi kwa washindi zikianikwa nao
wadau kujionea.
Mgeni rasmi wa siku ya Uzinduzi ni Katibu Mkuu wa TFF
Angetile Osiah.
Katika hatua nyingine kwa kutambua mchango wa
maendeleeo ya michezo nchini Kampuni ya My Way Entertainment ambao
ni waandaaji wa Meya's Cup 2013wamemwalika Mwanamichezo wa Sports Xtra Mbwiga
wa Mbwiguke....
Post a Comment