Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTANGAZAJI JOYCE KIRIA AOMBA AFAHAMISHWE ALIPO MUMEWE HENRY KILEO ...... CHEZEA MUME WEWE!!!



1aMtangazaji wa televisheni ya Chanel 5 EATV Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora na kupaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa 3Joyce Kiria akifafanua mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam huku akiwa amewabeba watoto wake na ndugu zake wengine wakiwa na mambongo yenye ujumbe mbalimbali 4Joyce Kiria akendelea kujibu maswali kadhaa ya wanahabari wakati akizungumza nao leo jijini dar es salaam.Habari Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog



Baada ya kukaa kwa siku mbili bila kujua alipo mume wangu, nimejitokeza mbele ya waandishi wa habari wapate kunisaidia kufikisha ujumbe wangu wa kupata msaada ya kujua mume wangu alipo.

Hapa ni karibu kabisa ya ukumbi wa habari maelezo ambapo niliwafuata waandishi wa habari ili kupata muda wa kuongea nao, nikiwa nimewabeba wanangu Lincon na Linston.

Nina watoto wawili mkubwa ni wa miaka 2 na mdogo wake ni wa miezi 4, leo ni siku ya nne hawajamuona baba yao, baba yao ni msaada mkubwa mno kwa familia yangu, Raisi Kikwete huko ulipo nakuomba usikie kilio changu, IGP Said Mwema nahitaji msaada wako, Wanawake na Wote nahitaji msaada wenu.


Hapa nikiendelea kuelezea hali halisi ya jambo hili mpaka leo hii kuja hapa, na kubwa ni kutopewa taarifa ya mume wangu alipo. Sina Amani kabisa naomba kupata taarifa kamili huko aliko yuko salama? na hata kufahamu anakula nini?

Kubwa watanzania wenzangu ni kunisaidia katika maombi ili huko aliko awe salama.

Kwa Urefu zaid habari hii itaruka katika vyombo mbalimbali vya habari zikiwepo TV kama Channel Ten, ITV, EATV, Star TV na Clouds, Radio kama Clouds, Radio One, na magazeti kama Mwananchi, Nipashe , Mtanzania, Tanzania Daima , The Citizen, Guardian, na vyombo vingine vya habari.

Nawashukuru waandishi wote ambao walikuwepo hapa, pia na watanzania wote naamini mko pamoja na mimi. .
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top