Miss Redds mkoa wa Singida,Nice Jack (katikati) Nice ni mwanafunzi wa chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida. Kushoto ni Mshindi wa pili,Abigael Mathias na kulia ni msindi watatu Aisha Abdul ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Singida.Washindi hao watatu,watashiriki shindao la miss Reds kanda ya kati.Kanda ya kati kwa upande wa sanaa ya urembo,inajumisha mikoa ya Singida,Dodoma, Tabora na Kigoma.
Na Nathaniel Limu
Mwanafunzi wa chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida, Nice Jack (19) ametawazwa kuwa Miss Reds mkoa wa Singida kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 baada ya kuwagaragaza warembo 12 waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.
Kwa ushindi huo,Nice amejipatia tiketi ya kushiriki shindano la Miss Reds kanda ya kati linalotarajiwa kufanyika wakati wowote mwezi huu mjini Dodoma.Pia Nice amezawadiwa shilingi laki nne kwa ushindi huo.
Nafasi ya pili imenyakuliwana Abigael Mathias (20), amepewa zawadi ya shilingi laki tatu na mwanafunzi mwingine wa chuo cha uhasibu,Aisha Abdul (19) ambaye ameshika nafasi ya tatu, ,amezawadiwa shilingi laki mbili. Mshindiwa pili na wa tatu, wanaungana na Miss Redds Mkoa wa Singida Nice, katika kushiriki shindano la Miss Redds Kanda ya kati.
Nafasi ya nne na tano zinachukuliwa na Joy Henry na Gloria Peter ambao kila mmoja, alizawadiwa shilingi laki moja.
Washindani wengine waliosalia kila mmoja alipewa kifuta jasho cha shilingi 80,000/=.
Akizungumza katika ufunguzi wa shindano hilo lililofanyika katika bwalo la shule ya sekondari Mwenge, mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Msindai aliwataka wazazi/walezi kuwasaidia watoto wao wa kike wenye sifa za kushiriki sanaa ya urembo, washiriki bila matatizo.
Msindai amesema sanaa ya urembo ni njia bora inayotoa fursa ya washiriki kujipatia kipato halali na ajira pia.

Post a Comment