Mzee Yasin Maluzuku akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake leo hii .
Mzee Yasin Maluzuku akionyesha sehemu yenye ufa katika ofisi yake
Hapa Mzee Yasin Maluzuku akiwa mbele ya nyumba yake
Mzee Yasin Maluzuku
Na Amon Mtega,Songea.
MWASISI wa chama cha mapinduzi CCM wa Kata ya Misufini Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma mzee Yasin Maluzuku amelalamikia uchakavu wa nyunba yake ambayo ipo hatarini kuanguka kufuatia uchakavu wa muda mrefu uliotokana na kutokufanyiwa matengenezo pamoja na nyumba hiyo kutumika kama ofisi ya chama cha mapinduzi tawi la Msikitini pia hawajapewa msaada wowote na chama pamoja na kukitumikia tangu enzi za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Maluzuku akiongea na mtandao huu nyumbani kwake alisema kuwa yeye amekitumikia chama hicho kwa muda mrefu tangu alipokutana na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi hii mwaka 1955 na kuwa ameshashika nyadifa mbali mbali za kiuongozi mpaka alipoamua kustaafu kwa sababu ya umri mwaka 2012 lakini chama bado hakijaonesha kuwajali kwa dhati wazee na hasa waasisi wa uhuru wa taifa hili.
Amesema kuwa mwalimu Nyerere wakati akipita kuelekea Nyasa alimuona mzee maluzuku kwenye kijiji kilichopo karibu na Nyasa na kumwambia ajiunge na chama cha TANU ndipo mzee huyo alikubali na kuanza kazi ya kusaka uhuru na alianza kazi hiyo kwa kubeba mizigo ya Mwalimu alipokuwa akifanya ziara Ruvuma.
Aidha pamoja na kupumzika kushika madaraka ndani ya chama hicho mzee huyo alisema kuwa ameamua kugawa chumba kimoja ndani ya nyumba yake kitumike kama ofisi ya CCM tawi la Msikitini baada ya kuona tawi hilo linahangaika mahali pa kufanyia kazi za kiofisi licha ya nyumba hiyo kuwa na dalili zote za kuanguka.
Maluzuku akiongelea upande wa rasimu ya katiba mpya iliyotoka sasa ambayo inaendelea kujadiliwa na wananchi mbali mbali amedai kuwa rasimu hiyo ni nzuri lakini inatakiwa ifanyiwe marekebisho madogo madogo hasa kwa upande wa muundo wa serikali tatu kwa sababu muundo huo utaligharimu Taifa na kuwa ulinzi wake utakuwa mgumu zaidi
Post a Comment